2 Wafalme 19 - Swahili Roehl Bible 1937

Hizikia anaomba wokovu kwa Bwana na kuupata.(Taz. Yes. 37; 2 Mambo 32:20-23.)

1Ikawa, mfalme Hizikia alipoyasikia, akazirarua nguo zake, akajifunga gunia, akaingia Nyumbani mwa Bwana.

2Akamtuma Eliakimu aliyekuwa mtunza nyumba ya mfalme na Sebuna aliyekuwa mwandishi na watambikaji wazee waliokuwa wamejifunga magunia kwenda kwa mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi.

3Wakamwambia: Hivi ndivyo, Hizikia anavyosema: Siku hii ya leo ni siku ya kusongwa na ya kupatilizwa na ya kutupwa, kwani watoto wamefikisha kuzaliwa, lakini nguvu za kuwazaa haziko.

4Labda Bwana Mungu wako ameyasikia yale maneno yote ya mkuu wa askari, ambayo bwana wake, mfalme wa Asuri, alimtuma kumbeua Mungu Mwenye uzima kwa kuyasema; Bwana Mungu wako na ampatilizie yale maneno, aliyoyasikia! Nawe na uje kuwaombea waliosalia walioko bado!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help