5 Mose 32 - Swahili Roehl Bible 1937

Wimbo wa Mose.

1Yasikilizeni, ninyi mbingu, nitakayoyasema!

Nawe nchi, yasikilize maneno ya kinywa changu!

2Mafunzo yangu na yatiririke kama maji ya mvua,

maneno yangu na yadondoke kama umande,,

kama manyunyu yanayonyunyiziwa majani mabichi,

kama matone ya mvua yanayotonea vijiti!

3Kwani nitalitangaza Jina la Bwana, nanyi mpeni ukuu aliye Mungu wetu!

4Ni mwamba, matendo yake humalizika, kwani njia zake zote huendelea sawa, ni Mungu mtegemevu asiye na upotovu, ni mwenye wongofu, tena ni mnyofu.

5Wasio watoto wake kwa kuwa wachafu, humfanyia mabaya, ndio kizazi chenye upotovu, hupenda kubisha.

7Zikumbuke siku za kale, uitambue miaka yao vizazi vilivyopita! Mwulize baba yako! Atakusimulia; waulize wazee! Nao watakuambia.

44Mose akenda, akayasema maneno yote ya wimbo huu masikioni pa watu, yeye na Yosua, mwana wa Nuni.

45Mose alipokwisha kuwaambia Waisiraeli wote maneno haya yote,

46akawaambia: Yawekeni mioyoni mwenu maneno haya yote, mimi ninayowashuhudia leo, nanyi mwaagize wana wenu, wayaangalie na kuyafanya maneno yote ya Maonyo haya!Mose anafumbuliwa na Bwana, atakapokufa.

48Siku iyo hiyo Bwana akamwambia Mose kwamba:

49Kwenye milima hii ya Abarimu uupande huo mlima wa Nebo ulioko katika nchi ya Wamoabu, unaoelekea Yeriko, uitazame nchi ya Kanaani, mimi nitakayowapa wana wa Isiraeli, iwe yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help