Yesaya 6 - Swahili Roehl Bible 1937

Utukufu wa Mungu unamtokea Yesaya.

1*Ule mwaka, mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana, akikalia kiti kirefu cha kifalme kilichowekwa juu, nazo nguo zake zikalijaza Jumba takatifu.

4Ikatetemeka hata misingi ya vizingiti kwa ukuu wa sauti yake aliyeyatangaza; nayo nyumba ikajaa moshi.Maneno, Yesaya aliyoagizwa kuyasema.

8Nikasikia sauti ya Bwana, akisema: Nitamtuma nani? Yuko nani atakayetuendea? Nikajibu: Mimi hapa! Nitume!*

9Akasema: Nenda, uwaambie watu wa ukoo huu kwamba:

Kusikia mtasikia, lakini hamtajua maana;

kutazama mtatazama, lakini hamtaona.

10Kwani mioyo yao walio ukoo huu uishupaze,

nayo masikio yao uyazibe,

nayo macho yao uyafumbe,

wasije wakaona kwa macho yao,

au wakasikia kwa masikio yao,

au wakajua maana kwa mioyo yao,

wakanigeukia, nikawaponya!

11Nikasema: Mpaka lini, Bwana? Akasema: Mpaka hapo, miji itakapokuwa mahame, kwa kuwa hamna mwenye kukaa humo, kwa kuwa nyumba hazina watu; mpaka hapo, nchi nayo itakapoangamia kwa kuwa mapori tu;

12mpaka hapo, Bwana atakapowapeleka watu mbali, mahame yawe mengi katika nchi hii.

13Tena kama sao litakuwa fungu la kumi tu, litaangamizwa mara nyingine. Litakuwa kama mkwaju au mtamba: ukikatwa, kunasalia shina lake; hilo shina lake litakuwa mbegu takatifu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help