Yosua 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Upande wa kaskazini wa Kanaani unatekwa.

1Ikawa, Yabini, mfalme wa Hasori, alipoyasikia, akatuma kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Simuroni na kwa mfalme wa Akisafu,

2na kwa wafalme waliokuwako kaskazini milimani na nyikani upande wa kusini wa Kineroti (Genezareti) na katika nchi ya tambarare na vilimani kwa Dori huko baharini,

3hata kwa Wakanaani waliokaa upande wa maawioni kwa jua na upande wa baharini na kwa Waamori na kwa Wahiti na kwa Waperizi na kwa Wayebusi milimani na kwa Wahiwi waliokaa chini kwa Hermoni katika nchi ya Misipa.

4Wakatoka wao pamoja na majeshi yao, wakawa watu wengi, kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari ulivyo mwingi; walikuwa hata na farasi na magari mengi sana.

5Hawa wafalme wote walipokwisha kupatana mashauri, wakaenda, wakapiga makambi pamoja kwenye ziwa la Meromu, wapate kupigana nao Waisiraeli.

6Lakini Bwana akamwambia Yosua: Usiwaogope! Kwani kesho saa zizi hizi mimi nitawatoa wao wote, kuwa wamekwisha kuuawa na Waisiraeli, nao farasi wao na uwakate mishipa, nayo magari yao na uyachome moto.

7Ndipo, Yosua na wapiga vita wote waliokuwa naye walipowaendea huko kwenye ziwa la Meromu, mara wakawashambulia,

8naye Bwana akawatia mikononi mwa Waisiraeli, wakawapiga, wakawakimbiza mpaka Sidoni ulio mkuu na mpaka Misirefoti-Maimu (Maji Kupwa) na mpaka bondeni kwa Misipe upande wa maawioni kwa jua, wakawapiga, wasisaze hata mmoja aliyekimbia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help