1Mtaona, siku ya Bwana ikija; ndipo, mateka yako yatakapogawanywa mjini mwako.Bwana Mungu atakaa Yerusalemu.
8Siku hiyo ndipo, maji yenye uzima yatakapotoka Yerusalemu, nusu yatakwenda katika bahari iliyoko maawioni kwa jua, nusu yatakwenda katika bahari nyingine; yatakuwa vivyo hivyo siku za kiangazi na siku za kipupwe.Mapatilizo ya adui.
12Hili ndilo pigo, Bwana atakaloyapiga makabila yote yaliyopeleka vikosi vyao kupigana na Yerusalemu: ataziozesha nyama za miili yao, wakiwa wamesimama kwa miguu yao, nayo macho yao yataoza ndani ya matundu yao, nazo ndimi zao zitaoza vinywani mwao.
13Tena siku hiyo ndipo, patakapokuwa kwao kitisho kikubwa kitokacho kwa Bwana, kila mtu akamate mkono wa mwenziwe, nao mkono wake yule utauinukia mkono wa mwenziwe.
14Wayuda nao watakuja kupigana mle Yerusalemu, mali za wamizimu wote pia wanaokaa na kuuzunguka zitakapokusanywa mle: dhahabu na fedha na nguo za sikukuu nyingi mno.
15Lile pigo litapiga vilevile nao farasi na nyumbu na ngamia na punda na nyama wote pia watakaokuwamo makambini mwao hao, liwe sawa na pigo lile la watu.
Utukufu wa ufalme wa Mungu.16Kisha masao ya wamizimu wote waliokuja kupigana na Yerusalemu watatoka kwao kuja kupanda papo hapo mwaka kwa mwaka, wamwangukie mfalme, ndiye Bwana Mwenye vikosi, na kuila sikukuu ya Vibanda.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.