Yohana 2 - Swahili Roehl Bible 1937

Arusi iliyokuwako Kana.

1*Siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya arusi huko Kana wa Galilea, hata mamake Yesu alikuwako,

2naye Yesu na wanafunzi wake wakaalikwa arusini.

3Mvinyo ilipopunguka, mamake Yesu akamwambia: Hawana mvinyo.

4Yesu akamwambia: Mama, tuko na jambo gani, mimi na wewe? Saa yangu haijaja bado.

12Kisha wakashuka kwenda Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake, wakakaa huko siku zisizokuwa nyingi.Kuwafukuza wachuuzi Patakatifu.

13*Pasaka ya Wayuda ilipokuwa karibu, Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.

(14-16: Mat. 21:12-13; Mar. 11:15-17; Luk. 19:45-46.)

14Alipoona hapo Patakatifu wenye kuuzia palepale ng'ombe na kondoo na njiwa, hata wavunjaji wa fedha waliokuwapo wamekaa,

15akaokota kamba, akazisuka kambaa, akawafukuza wote hapo Patakatufu, hata kondoo na ng'ombe, akazimwaga fedha za wavunjaji na kuziangusha meza zao.

16Wenye kuuza njiwa akawaambia: Yaondoeni haya hapa! Msiigeuze Nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya uchuuzi!

17Hapo wanafunzi wake wakakumbuka, ya kuwa imeandikwa:

18Kwa ajili ya Nyumba yako wivu unanila!* Wayuda walipomwuliza wakimwambia: Unatuonyesha kielekezo gani, kwa kuwa unafanya hivyo?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help