2 Timoteo 2 - Swahili Roehl Bible 1937

Askari mwema wa Kristo.

1Basi wewe mwanangu, ujipatie nguvu, tunazogawiwa tukiwa wake Kristo Yesu!

2Nayo mambo, uliyoyasikia kwangu mbele yao wengi waliosikiliza, hayo uwalimbikishe watu welekevu watakaoweza kufundisha hata wengine.

3Vumilia ukiteswa vibaya pamoja nami, kama inavyompasa askari mzuri wa Kristo Yesu!Kuepusha wapuzi.

14Wakumbushe mambo hayo na kuwaonya mbele yake Mungu, wasibishane! Maana haifai kitu, huwapotoa tu wenye kusikiliza.1 Tim. 6:4; Tit. 3:9.

15Jipingie kujitokeza kwa Mungu kuwa mfanya kazi aliye wa kweli, asiyefanya mambo yenye soni, anayelilinganisha vema neno la kweli, atakalogawia watu!1 Tim. 4:6; Tit. 2:7-8.

16Lakini penye upuzi wa bure usio na maana uepuke! Kwani wako watakaoendesha mambo ya kumbeza Mungu,1 Tim. 4:7.

17nalo neno lao litaambukiza kama ukoma; miongoni mwao hao wamo Himeneo na Fileto1 Tim. 1:20.

18waliopotelewa nayo yaliyo ya kweli wakisema: Ufufuko umekwisha kuwapo. Ndivyo, walivyokosesha hata wengine, wasimtegemee Bwana tena.

19Lakini msingi, Mungu aliouweka, uko, umeshupaa vivyo hivyo, hujulikana kwa muhuri yake, ni hii: Bwana huwatambua walio wake! Tena: Kila mwenye kulitambikia Jina la Bwana atenguke penye upotovu!4 Mose 16:5; Yoh. 10:14,27.

20Katika nyumba kubwa hamna vyombo vya dhahabu au vya fedha tu, ila vimo hata vyombo vya miti na vya udongo; navyo vingine ni vya mapambo, vingine ni vya machafu.

21Mtu akiwaepuka wale watu, asijichafue, atakuwa chombo cha pambo kilichotakaswa, naye mwenye nyumba atakitumia, maana kimefalia kazi zote zilizo njema.

Kuzikimbia tamaa.

22Tamaa za ujana zikimbie, ukimbilie kupata wongofu na kumtegemea Mungu na kupendana na kupatana nao wote wanaomtambikia Bwana kwa mioyo itakatayo!1 Tim. 6:11.

23Lakini mabishano ya upuzi wa watu wasioonyeka yakatae! Jua, ya kuwa huleta magombano tu!1 Tim. 4:7.

24Lakini aliye mtumwa wa Bwana haimpasi kugombana, sharti awaendee wote kwa unyenyekevu akijua kuwafundisha, akivumilia wenye uovu.Tit. 1:7.

25Akiwa mpole hivyo ataweza kuwaonya wapingani nao, kama Mungu anawajutisha, wayatambue yalio ya kweli;

26kisha watalevuka, wajinasue matanzini mwa Msengenyaji, ambaye walinaswa naye, wamfanyizie, ayatakayo yeye.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help