4 Mose 14 - Swahili Roehl Bible 1937

Waisiraeli wanapatiliziwa manung'uniko yao, wakae nyikani miaka arobaini.(Taz. 5 Mose 1:26-44.)

1Ndipo, wao wote wa mkutano walipozipaza sana sauti zao, watu wakalia usiku kucha.

2Wana wote wa Isiraeli wakamnung'unikia Mose na Haroni, nao wote walio wa mkutano wao wakawaambia: Afadhali tungalikufa katika nchi ya Misri au tungekufa huku nyikani!

11Bwana akamwambia Mose: Watu hawa watanitukana mpaka lini? Watakataa mpaka lini kunitegemea? Nami nimevifanya hivyo vielekezo vyote kwao!

12Nitawapiga kwa ugonjwa mbaya uuao, niwatoweshe, kisha nitakufanya wewe kuwa kabila kubwa lenye nguvu kuliko hawa.

39Mose alipowaambia wana wote wa Isiraeli maneno haya, wakasikitika sana.

40Kesho yake wakaamka na mapema, wakapanda mlimani juu kileleni na kusema: Basi, tumekwisha kufika huku, sasa twende kupanda mahali pale, Bwana alipotuelekeza! Kwani tumekosa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help