1 Watesalonike 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Anawaonya, watakate.

1*Pamesalia, ndugu, tuwahimize na kuwabembeleza, kwa hivyo, mlivyo wake Bwana Yesu, mfanye mwenendo uwapasao wa kumpendeza Mungu ulivyo.

2Kwani mwayajua maagizo, tuliyowaagiza, kama tulivyoyapata kwake Bwana Yesu.

3Kwani haya ndiyo, Mungu ayatakayo: mtakaswe, mwuepuke ugoni.

4Kila mmoja wenu ajue kuuangalia mwili wake, uwepo ukitakata na kupata heshima iupasayo,Upendano sharti ukue.

9Kwa ajili ya upendano ninyi hampaswi na kuandikiwa neno, kwani ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.Kufufuka na kumwona Bwana.

13*Lakini, ndugu, hatutaki, ninyi mkose kujua, mambo yao waliolala yalivyo, msione masikitiko kama wale wengine wasio na kingojeo.1 Kor. 15:20; Ef. 2:12.

14Kwani tukiyategemea, ya kuwa Yesu alikufa, kisha akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu nao waliolala katika Yesu atawapeleka, wawe pamoja naye.Rom. 14:9; 1 Kor. 15:3-4,12.

15Kwani neno hili, tunalowaambia, ni neno lake Bwana kwamba: Sisi tunaoishi, tuliosazwa, mpaka Bwana atakapokuja, hatutawatangulia wale waliolala.Mat. 16:28; 24:30-31; 1 Kor. 15:51.

16Kwani Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni papo hapo, wito utakapovumika, nayo sauti ya malaika mkuu itasikilika, hata baragumu la Mungu litalia. Ndipo, waliokufa katika Kristo watakapofufuka kwanza;1 Kor. 15:23,52.

17kisha sisi tuliosazwa, tutakaokuwa tu hai, tutapokonywa katika mawingu pamoja nao hao, tupate kukutana na Bwana angani. Hivyo tutakuwa pamoja na Bwana siku zote.Yoh. 12:26; 17:24.

18Tulizaneni mioyo ninyi kwa ninyi na kisimuliana maneno haya!*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help