Luka 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Kujaribiwa kwa Yesu.(1-13: Mat. 4:1-11; Mar. 1:12-13.)

1Yesu akajaa Roho takatifu, akarudi akitoka huko Yordani, akapelekwa na Roho nyikani,

2akajaribiwa siku 40 na Msengenyaji. Siku zile hakula cho chote; zilipokwisha pita, akaona njaa.

3Msengenyaji akamwambia: Kama ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili, liwe chakula!

4Yesu akamjibu akisema: Imeandikwa:

Mtu hataishi kwa chakula tu, ila kwa kila neno la Mungu.

11nao watakuchukua mikononi mwao,

usije kujikwaa mguu wako katika jiwe.

12Yesu akajibu akimwambia: Liko neno la kwamba:

Usimjaribu Bwana Mungu wako!Mahubiri katika Nasareti.(14-15: Mat. 4:12-17; Mar. 1:14-15.)

14Yesu akarudi Galilea mwenye nguvu ya Roho, akavumika katika nchi zote zilizoko pembenipembeni.

15Naye alipofundisha katika nyumba zao za kuombea akatukuzwa nao wote.

(16-30: Mat. 13:53-58; Mar. 6:1-6.)

16*Alipofika Nasareti, - ndio mji, alimolelewa, - akaingia siku ya mapumziko nyumbani mwa kuombea, kama alivyozoea. Alipoinuka kuwasomea

17akapewa kitabu cha mfumbuaji Yesaya; alipokifunua hicho kitabu akaona mahali palipolandikwa:

18Roho ya Bwana inanikalia,

kwa hiyo ameanipaka mafuta,

niwapigie maskini mbiu njema.

Amenituma, niwatangazie mateka,

ya kuwa watakombolewa,

nao vipofu, ya kuwa wataona,

niwape ruhusa walioumizwa, wajiendee,

19niutangaze mwaka wa Bwana upendezao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help