Iyobu 7 - Swahili Roehl Bible 1937

Iyobu anamwomba Mungu, amwue, ayakomeshe mateso yake.

1Je? Mtu hashurutishwi kufanya kazi ya vita huku nchini? Siku zake si sawa kama siku zake mkibarua?

11Kwa hiyo mimi sitakizuia kinywa changu, niseme kwa kusongeka rohoni mwangu, nilie kwa uchungu wa moyo wangu.

12Je? Mimi ni kama bahari au kama nyangumi, ukiniwekea watu wa kuniangalia?

13Nikisema: Kilalo changu ndicho kitakachonituliza moyo, kitanda changu kitanipunguzia vilio vyangu,

14ndipo, unaponitisha kwa kuniotesha ndoto, kwa kunionyesha maono unanistusha.

15Kwa hiyo roho yangu inapenda kunyongwa tu, kuliko kuwa gofu la mtu, kama nilivyo, inapenda kufa kweli.

16Nimekata tamaa kwa kukataa kuwapo kale na kale; kwa sababu siku zangu ni za bure, uniache tu!1 Fal. 19:4.

17Mtu ndio nini, ukimkuza, ukimwelekezea moyo wako, umwangalie?Iy. 14:1-5; Sh. 8:5.

18Ukimkagua kila kunapokucha? Ukimjaribu punde kwa punde?

19Mbona hutakoma kunitazama? Hutaniacha peke yangu, niyameze mate yangu?

20Kama nimekosa, nimekufanyia nini, wewe mlinda watu? Mbona umeniweka kuwa shabaha yako ya kuipiga, mpaka nikijiona mwenyewe kuwa mzigo?

21Mbona huniondolei maovu yangu, ukazitowesha nazo manza, nilizozikora? Kwani sasa ninakwenda zangu kulala uvumbini; utakaponitafuta mapema utaniona, sipo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help