4 Mose 21 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumshinda mfalme wa Aradi.

1Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyekaa upande wa kusini aliposikia, ya kuwa Waisiraeli wanakuja wakiifuata njia ya wapelelezi, akapigana nao Waisiraeli, akateka wengine wa kwao.

2Ndipo, Waisiraeli walipomwapia Bwana kiapo cha kwamba: Ukiwatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza miji yao kwa kuitia mwiko wa kuwapo.Nyoka ya shaba.

4Kisha wakaondoka kwenye mlima wa Hori wakishika njia ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu, waizunguke nchi ya Edomu. Watu walipotaka kuzimia roho kwa kuchoka njiani,

5wakamgombeza Mungu, hata Mose kwamba: Kwa nini mlitutoa Misri, tujifie huku nyikani? Kwani hakuna chakula wala maji, nazo roho zetu zinachukizwa na chakula hiki kikosacho nguvu.

6Ndipo, Bwana alipotuma nyoka za moto kuwajia hao watu; nao walipowauma watu, wakafa watu wengi kwao Waisiraeli.

15Bonde la Sufa na vijito vya Arnoni,

napo vijito vinaposhukia,

panapopafikia napo mahali penye mji wa Ari

ndipo panapouegemea mpaka wa Moabu.

16Toka hapo wkafika Kisimani;

ndiko kwenye kile kisima, Bwana

alikomwambia Mose kwamba: Wakusanye watu, niwape maji!

17siku zile Waisiraeli waliuimba wimbo huu:

18Bubujika, kisima! Haya! Kiimbieni!

Waliokichimba kisima hiki ndio wakuu;

kweli majumbe wa watu ndio waliokifukua.

kwa kutumia bakora na fimbo zao za kifalme.

Toka huko nyikani wakaenda Matana.

19Toka Matana wakaenda Nahalieli, toka Nahalieli wakaenda Bamoti,

20toka Bamoti wakaenda bondeni kwenye mbuga za Moabu zilizoko kwenye mlima na Pisiga uelekeao jangwani.

Kumshinda Sihoni.

21Waisiraeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni, mfalme wa Waamori, kwamba:

30Tulipowapiga mishale, ndipo, Hesiboni ulipoangamia mpaka Diboni, tukaiharibu nchi mpaka Nofa, tukafika hata Medeba.

31ndipo, Waisiraeli walipokaa katika nchi ya Waamori.

Kumshinda Ogi.

32Kisha Mose akatuma watu kwenda Yazeri kupeleleza, nao wakaiteka mitaa yake na kuwafukuza Waamori waliokuwamo.

33Kisha wakageuka, wakaishika njia ya kupanda Basani. Lakini Ogi, mfalme wa Basani, akatoka kuwazuia, yeye na watu wake wote, wakapigana huko Edirei.5 Mose 3:1-11.

34Bwana akamwambia Mose: Usimwogope, kwani nimemtia mkononi mwako pamoja na watu wake wote, hata nchi yake, umfanyizie, kama ulivyomfanyizia Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni.Sh. 136:17,22.

35ndipo, walipompiga yeye na wanawe na watu wake wote, wasisaze kwake hata mmoja aliyeweza kukimbia, kisha wakaitwaa nchi yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help