Waamuzi 17 - Swahili Roehl Bible 1937

Mika anatengeneza kinyago.

1Milimani kwa Efuraimu kulikuwa na mtu, jina lake Mika.

7Kulikuwa na kijana wa Beti-Lehemu wa Yuda uliokuwa wa ukoo wa Yuda, naye alikuwa Mlawi, lakini alikuwa mgeni huko.Amu. 18:3.

8Kisha huyu mtu akaondoka katika mji wa Beti-Lehemu wa Yuda kwenda kukaa ugenini mahali, atakapopaona; naye akafika milimani kwa Efuraimu nyumbani kwa Mika alipokuwa anajiendea tu.

9Mika akamwuliza: Umetoka wapi? Naye akamwambia: Mimi ni Mlawi wa Beti-Lehemu wa Yuda, nimekwenda kukaa ugenini mahali, nitakapopaona.

10Mika akamwambia: Kaa kwangu, uniwie baba na mtambikaji! Nami nitakupa fedha kumi mwaka kwa mwaka, hata nguo za kuvaa na vyakula vya kukutunza nitakupatia. Huyu Mlawi kwanza alitaka kwenda zake,

11halafu ikampendeza huyu Mlawi kukaa kwa huyu mtu, kisha huyu kijana akawa kwake kama mwanawe mmoja.

12Mika akamjaza gao huyu Mlawi, ndipo, huyu kijana alipokuwa mtambikiaji wake, akakaa nyumbani mwa Mika.

13Naye Mika akasema: Sasa najua, ya kuwa Bwana atanifanyizia mema, kwa kuwa huyu Mlawi ni mtambikaji wangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help