1Wafilisti wakavikusanya vikosi vyao vyote Afeki, nao Waisiraeli wakapiga makambi yao kwenye chemchemi iliyoko Izireeli.
6Ndipo, Akisi alipomwita Dawidi, akamwambia: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, wewe u mtu mnyofu! Kwa hiyo ilifaa machoni pangu, utoke pamoja nami, uingie katika vita hivi pamoja nami, kwani sikuona kwako kibaya cho chote tangu siku hiyo, ulipokuja kwangu, hata siku hii ya leo; lakini machoni pao wakuu wewe hufai.
7Sasa rudi, ujiendee na kutengemana, usifanye kilicho kibaya machoni pao wakuu wa Wafilisti!
8Ndipo, Dawidi alipomwambia Akisi: Nimefanya nini? Au umeona nini kwa mtumishi wako tangu siku hiyo, nilipokutokea, hata siku hii ya leo, nisije kupiga vita nao adui wa bwana wangu mfalme?
9Akisi akamjibu na kumwambia: Ninakujua, ya kuwa wewe u mwema machoni pangu kama malaika wa Mungu; ni wao wakuu wa Wafilisti waliosema: Asipande pamoja nasi kupiga vita!2 Sam. 19:27.
10Sasa uamke na mapema! Nao watumishi wa bwana wako waliokuja pamoja nawe nanyi mwamke na mapema, mkipata kuona, mwende zenu!
11Kwa hiyo yeye Dawidi na watu wake wakaamka na mapema kwenda zao, warudi katika nchi ya Wafilisti, nao Wafilisti wakapanda kwenda Izireeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.