1Ilipokuwa asubuhi, watambikaji wakuu wote na wazee wa kwao wakamlia Yesu njama, kwamba wamwue.(15-26: Mar. 15:6-15; Luk. 23:13-25; Yoh. 18:39-19:1.)
15*Kwa desturi ya sikukuu mtawala nchi alikuwa amezoea kuwafungulia mfungwa mmoja, watu wengi waliyemtaka.
16Siku zile palikuwa na mfungwa aliyejulikana kwa ubaya, jina lake Baraba.
17Walipokusanyika, Pilato akawauliza: Mwamtaka yupi, niwafungulie? Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?
18Kwani aliwajua, ya kuwa wamemtoa kwa wivu.
19Naye alipoketi katika kiti cha uamuzi, mkewe akatuma kwake kumwambia: Usijitie katika jambo la yule mwongofu! Kwani nimeteseka mengi kwa ajili yake katika ndoto za usiku wa leo.
20Lakini watambikaji wakuu na wazee wakawashurutisha makundi ya watu, wamtake Baraba, wamwangamize Yesu.
21Mtawala nchi akajibu akiwaambia: Katika hawawawili mwamtaka yupi, niwafungulie? Wakasema: Baraba!
22Pilato akamwambia: Basi, Yesu anayeitwa Kristo nimfanyie nini? Wakasema wote: Na awambwe msalabani!
23Aliposema: Ni kiovu gani, alichokifanya? wakakaza kupiga makelele wakisema: Na awambwe msalabani!
24Pilato alipoona, ya kama hakuna linalofaa, ila matata yatakuwako mengi, akatwaa maji, akanawa mikono yake machoni pa watu, akasema: Mimi simo katika damu ya mtu huyu mwongofu, tazameni, ni shauri lenu!
39Waliopita wakamtukana, wakavitingisha vichwa vyaoKuzikwa.(57-61: Mar. 15:42-47; Luk. 23:50-55; Yoh. 19:38-42.)
57Ilipokuwa jioni, akaja mtu mwenye mali nyingi wa Arimatia, jina lake Yosefu; naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.