1Ninyi mlio ukoo wangu, yasikilizeni mafundisho yangu! Yategeni masikio yenu, msikie, kinywa changu kinavyoyasema!
2Nitakifumbua kinywa changu, kiseme mifano na kuwaambia mafumbo yaliyo ya kale.
32Katika mambo hayo yote wakamkosea tena, hata vioja vyake hawakuvitegemea.
33Kwa hiyo alizimaliza siku zao upesi, wakawa kama mvuke, miaka yao ikapita upesi sana, alipowaangamiza kwa mastuko.
34Napo hapo, alipowaua hivyo, ndipo, walipomtafuta, wakarudi na kumtazamia machana kutwa.
40Je? Mara ngapi walimchokoza nyikani, wakamsikitisha jangwani?
54Akawafikisha kwenye mpaka wa Patakatifu pake, penye ule mlima, ambao ulijipatia mkono wake wa kuume.
65Kisha Bwana aliamka kama mtu aliyelala usingizi, kama mwenye nguvu anayepiga shangwe akiondoka kwenye mvinyo.
66Akawapiga waliowasonga, akawarudisha nyuma, nayo masimango ya kale na kale ndiyo, aliyowapatia.
67Akakitupa kituo cha Yosefu, nao ukoo wa Efuraimu hakuuchagua.Sh. 78:9.
68Akauchagua ukoo wa Yuda na mlima wa Sioni, alioupenda.2 Mambo 6:6.
69Akapajenga Patakatifu pake, paende juu kabisa, pawe kama nchi, aliyoiweka ya kuwapo kale na kale.
70Kisha akamchagua mtumishi wake Dawidi, aje kumtumikia; kwenye mazizi ya kondoo ndiko, alikomchukua.1 Sam. 16:11-12.
71akamtoa kwenye kondoo wanyonyeshao, awachunge walio ukoo wake Yakobo pamoja nao walio fungu lake Isiraeli.2 Sam. 7:8.
72Akawachunga kwa kuwa mwenye moyo uliotakata wote, kwa kuwa mikono yake iliijua kazi hiyo, akawaongoza.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.