Mashangilio 76 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumtukuza Mungu, kwa kuwa ni mshindaji.

1Kwa mwimbishaji, wa kuimbia mazeze. Wimbo wa Asafu wa kushukuru.

4Kwa utukufu wako wewe unaogopesha, maana huipita ile milima ya wanyang'anyi kwa kuwa mkubwa.

5Wenye mioyo mikali walitekwa nao, wakalala usingizi kwa kuangushwa wale wenye nguvu wote pia, mikono yao ikawalegea.

6Kwa makaripio yako, Mungu wa Yakobo, waliomo garini waliangushwa, wakazimia roho pamoja na farasi.

7Wewe unaogopesha kweli; atakayesimama mbele yako wewe, moto wa makali yako ukitokea, atapatikana wapi?

8Ulipotangaza maamuzi toka mbinguni, nchi ikashikwa na woga, ikanyamaza kimya;Sh. 46:11; Hab. 2:20.

9ndipo, Mungu alipoinuka kuwaamulia watu, apate kuwaokoa wanyonge wote walioko nchini.

10Kwani makali ya watu nayo hukutukuza, mwisho utauzima nao moto wa makali yao utakapojifunga.

11Mkimwapia, mlipeni Bwana Mungu wenu! Wote wakaao na kumzunguka sharti wampelekee matunzo, kwani yeye hutisha, aogopwe sana,2 Mose 15:11; 5 Mose 7:21.

12huzikata roho zao walio wakuu, nao wafalme wa nchi huwaogopesha.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help