5 Mose 6 - Swahili Roehl Bible 1937

Maelezo ya Agano la kwanza.

1Nayo haya ndiyo maagizo na maongozi na maamuzi, Bwana Mungu wenu aliyoniagiza, niwafundishe ninyi, mpate kuyafanya katika nchi, mnayoivukia kuichukua, iwe yenu.

2Sharti umwogope Bwana Mungu wako, uyaangalie maongozi na maagizo yake yote, ninayokuagiza, wewe na wanao na wana wa wanao siku zote za maisha yako, kusudi siku zako zipate kuwa nyingi.

3Isiraeli, yasikie na kuyaangalia, uyafanye, kusudi uone mema, nanyi mpate kuwa wengi sana, kama Bwana Mungu wa baba zako alivyokuagia kukupa nchi ichuruzikayo maziwa na asali.

4*Sikia, Isiraeli: Bwana Mungu wetu ni Bwana peke yake.

16Msimjaribu Bwana Mungu wenu, kama mlivyomjaribu kule Masa.

20Mwanao atakapokuuliza siku zijazo kesho kwamba: Nini maana yao haya mashuhuda na maongozi na maamuzi, Bwana Mungu wetu aliyowaagiza ninyi?2 Mose 13:14.

21ndipo umwambie mwanao: Sisi tulikuwa watumwa wa Farao kule Misri, lakini Bwana akatutoa Misri kwa mkono wake wenye nguvu,

22Bwana alipofanya machoni petu kule Misri vielekezo na vioja vikubwa vilivyomwogopesha Farao na mlango wake wote.

23Ndivyo, alivyotutoa huko na kutuleta huku, atupe nchi hii, aliyowaapia baba zenu.

24Ndipo, Bwana alipotuagiza kuyafanya haya maongozi yote kwa kumcha Bwana Mungu wetu, tuone mema siku zote za maisha yetu, kama inavyoelekea leo.

25Nao wongofu wetu ndio huu wa kujiangalia, tuyafanye haya maagizo yote mbele ya Bwana Mungu wetu, kama alivyotuagiza.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help