1Ikawa, Isaka alipokuwa mkongwe, macho yake yakatenda kiza, yasione; ndipo, alipomwita mwanawe mkubwa Esau, akamwambia: Mwanangu! Naye akamwitikia: Mimi hapa!
2Akasema: Tazama, nimekuwa mkongwe, siijui siku ya kufa kwangu.
3Sasa yachukue mata yako, ndio podo lako na upindi wako, uende porini kuniwindia nyama!
4Kisha unitengenezee kilaji cha urembo, kama ninavyokipenda, uniletee, nile, roho yangu ipate kukubariki, nikingali bado sijafa.
5Lakini Rebeka alikuwa ameyasikia, Isaka aliyomwambia mwanawe Esau. Esau alipokwisha kwenda porini kuwinda nyama ya kumpelekea baba,
6Rebeka akamwambia mwanawe Yakobo kwamba: Tazama, nimesikia, baba yako akimwambia kaka yako Esau kwamba:
7Niletee nyama ya porini, unitengenezee kilaji cha urembo, nile, nipate kukubariki usoni pa Bwana kabla ya kufa kwangu!
8Sasa mwanangu, isikie sauti yangu, uyafanye nitakayokuagiza!
9Nenda makundini kunichukulia huko wana wawili wa mbuzi walio wazuri, nimtengenezee baba yako nyama zao kuwa kilaji cha urembo, kama anavyokipenda.
10Kisha utampelekea baba yako, ale, apate kukubariki kabla ya kufa kwake.
11Lakini Yakobo akamwambia mama yake Rebeka: Tazama, kaka yangu Esau ni mwenye manyoya, lakini mimi sinayo.
30Ikawa, Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, naye Yakobo alipokwisha kutoka usoni pa baba yake Isaka, ndipo, kaka yake Esau aliporudi kwa kuwinda.
31Naye akatengeneza kilaji cha urembo, akampelekea baba yake, akamwambia baba yake: Baba, inuka, ule nyama, mwanao alizokuwinda, roho yako ipate kunibariki!
32Ndipo, baba yake Isaka alipomwuliza: Wewe ndiwe nani? Akajibu: Mimi ni mwanao wa kwanza Esau.
33Ndipo, Isaka aliposhangaa mshangao mkubwa mno, akasema: Sasa ni nani yule mwinda nyama aliyeniletea nyama, nikala, ulipokuwa hujaja bado, nikambariki? Naye atakuwa amebarikiwa.
34Esau alipoyasikia haya maneno ya baba yake, akalia kilio kikubwa chenye uchungu mwingi sana, akamwambia baba yake: Baba, nibariki mimi nami!Esau anataka kumwua Yakobo.
41Esau akamchukua Yakobo kwa ajili ya hiyo mbaraka, baba yake aliyombariki; kwa hiyo Esau akasema moyoni mwake: Siku za kumwombolezea baba ziko karibu; zitakapopita, nitamwua ndugu yangu Yakobo.
42Rebeka alipopata habari ya lile shauri la mwananwe mkubwa Esau, akatuma kumwita mwanawe mdogo Yakobo, akamwambia: Tazama! Kaka yako Esau anajituliza moyo kwa kwamba, akuue.
43Sasa mwnanangu, isikie sauti yangu! Inuka, ukimbilie Harani kwa kaka yangu Labani!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.