1 Samweli 23 - Swahili Roehl Bible 1937

Dawidi anauokoa mji wa Keila.

1Watu wakamsimulia Dawidi kwamba: Wafilisti wanapiga vita huko Keila, nao hunyang'anya yaliyopo penye kupuria.Dawidi anaokolewa katika nyika ya Maoni, Sauli asimpate.

19Kulikuwako Wazifu waliopanda Gibea kwa Sauli kumwambia: Je? Dawidi hajifichi kwetu magengeni mwituni katika kilima cha Hakila kilichoko kusini kwenye jangwa?1 Sam. 26:1; Sh. 54:2.

20Sasa wewe mfalme, shuka tu kwa hivyo, roho yako inavyotamani kabisa kushuka! Nasi tutamtoa, tumtie mkononi mwa mfalme.

21Sauli akasema: Na mbarikiwe na Bwana, kwa kuwa mmenihurumia!

22Nendeni kumvumbua tena, mpate kujua na kupaona mahali pake panapo nyayo zake, mmjue naye aliyemwona. Kwani watu huniambia, ya kuwa ni mwerevu sanasana.

23Tazameni, myajue maficho yote pia, anamojificha! Kisha rudini kwangu kwa hayo, mliyoyavumbua, nipate kwenda nanyi! Kama yuko katika nchi hii, nitamtafuta, nimpate katika maelfu yote ya Yuda.

24Kisha wakaondoka, wakaenda Zifu mbele ya Sauli; lakini Dawidi na watu wake walikuwa porini katika nyika ya Maoni upande wa kusini kwenye jangwa.

25Sauli alipokwenda na watu wake kumtafuta, watu wakampasha Dawidi habari; ndipo, aliposhuka mwambani, akakaa katika nyika ya Maoni. Sauli aliposikia, akaja upesi kumfuata kule nyikani kwa Maoni.

26Sauli akashika njia ya upande wa huku wa mlima ule, naye Dawidi na watu wake wakashika njia ya upande wa huko wa mlima uleule, lakini Dawidi akajihimiza kumkimbia Sauli. Hapo, Sauli na watu wake walipomfikia Dawidi na watu wake na kuwazunguka, wawakamate,

27ndipo, mjumbe alipofika kwa Sauli kwamba: Uje mbiombio, kwani Wafilisti wanaiteka nchi hii!

28Ndipo, Sauli alipoacha kumkimbiza Dawidi, akawageukia Wafilisti, kwa hiyo wakapaita mahali pale Mwamba wa Matengano.

29Kisha Dawidi akaondoka hapo, akakaa magengeni huko Engedi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help