1 Mose 34 - Swahili Roehl Bible 1937

Dina na Sikemu wanakosa.

1Dina, binti Lea, ambaye alimzalia Yakobo, akatoka kuwatazama wanawake wa nchi hiyo.

13Ndipo, wana wa Yakobo walipomjibu Sikemu na baba yake Hamori kwa udanganyifu, kwa kuwa alimchafua umbu lao Dina;

14kwa hiyo wakasema na kuwaambia: Hatuwezi kulifanya jambo hili, tumpe mtu mwenye govi umbu letu, kwani hivi vitatutia soni.

15Tutaweza kuwaitikia neno hilo hapo tu, mtakapokuwa kama sisi, kwenu wa kiume wote wakitahiriwa.

16Ndipo, tutakapowapa wana wetu wa kike, tujichukulie nao wana wenu wa kike, tukae pamoja nanyi kuwa kabila moja.

17Lakini msipotusikia na kutahiriwa, tutamchukua mtoto wetu, twende zetu.

18Haya maneno yao yakawa mema machoni pake Hamori napo machoni pake Sikemu, mwana wa hamori.

19Huyu kijana hakukawa kulifanya neno hilo, kwani alipendezwa naye binti Yakobo; naye alikuwa mwenye macheo kuliko wote a mlango wa baba yake.

20Hamori na mwanawe Sikemu walipofika langoni pa mji wao wakasema na watu wa mji wao kwamba:

21Watu hawa wanataka kukaa kwetu katika nchi yetu na kutengemana, wachuuzie huku; nanyi mnaiona nchi hii kuwa pana huku na huko, waenee nao; wana wao wa kike tutajichukulia kuwa wake zetu, nao wana wetu wa kike tutawapa wao.

22Lakini liko neno moja, watu hawa wanalolitaka, wapate kutuitikia na kukaa kwetu, tuwe kabila moja, ni hili: Kwetu wa kiume wote watahiriwe, kama wenyewe walivyotahiriwa.

23Je? Hivyo makundi yao na mapato yao na nyama wote, wanaowafuga, hawatakuwa mali zetu sisi? Kwa hiyo na tuwaitikie, wakae kwetu!

24Wote waliotoka langoni pa mji wakamsikia Hamori na mwanawe Sikemu, wakatahiriwa wa kiume wote pia, ndio wao wote waliotoka langoni pa mji wake.

Waume wote wa Sikemu wanauawa.

25Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wanaumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua kila mtu upanga wake, wakaingia mle mjini, watu walimokaa na kutulia, wakawaua wa kiume wote.1 Mose 49:5-7.

26Naye Hamori na mwanawe Sikemu wakawaua kwa ukali wa panga, kisha wakamchukua Dina nyumbani mwa Sikemu, wakatoka kwenda zao.

27Ndipo, wana wengine wa Yakobo walipowajia wale waliouawa, wakaziteka mali za humo mjini, kwa kuwa walimchafua umbu lao.

28Wakawachukua mbuzi na kondoo wao na ng'ombe wao na punda wao nayo yaliyokuwamo mjini nayo yaliyokuwako mashambani.

29Wakateka mali zao zote na wana wao wote na wake zao, nayo yote yaliyokuwamo nyumbani wakayanyang'anya.

30Naye Yakobo akamwambia Simeoni na Lawi: Mmenipatia mabaya, mmefanya mnuko wangu kuwa mbaya kwao wanaokaa katika nchi hii, kwa Wakanaani na Waperizi, nami watu wangu wanahesabika upesi. Watakaponikusanyikia, watanipiga; ndivyo, nitakavyotoweka mimi na mlango wangu.2 Mose 5:21.

31Lakini wakasema: Je? Tungeacha tu, amtumie umbu letu kama mwanamke mgoni?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help