1Ndugu zangu, haifai, wengi wakiwa wafunzi. Jueni: hukumu, tutakayoipata sisi, itakuwa kuliko ya wengine!
2Kwani sisi sote hukosa mengi. Mtu asipokosa kwa kusema, huyo ni mume mtimilifu anayeweza kuuongoza hata mwili wote.
3Tazameni, farasi twawatia hatamu vinywani, watutii sisi; nasi hivyo huwaongoza miili yao yote kwenda huko, tunakopenda.
4Tazameni, hata merikebu zilivyo kubwa sana, tena zinavyochukuliwa na pepo zenye nguvu! Nazo huongozwa na sukani iliyo ndogo sana, mwenye kuishika anakotaka.
5Vivyo hivyo nao ulimi ni kiungo kidogo, nao hujivunia makuu! Tazameni, moto ulio mdogo huchoma pori kubwa!
6Nao ulimi ni moto, ni ulimwengu wenye upotovu. Katika viungo vyetu ndio ulimi unaouchafua mwili wote, unavichoma vyote vilivyoumbwa, wenyewe ukiwashwa na moto ulioko kuzimuni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.