1Dawidi akasema moyoni mwake kwamba: Siku moja nitaangamizwa kwa mkono wa Sauli; sitaona mema, nisipojiponya kabisa na kuikimbilia nchi ya Wafilisti, Sauli akate tamaa za kunitafuta tena katika mipaka yote ya Waisiraeli; ndivyo, nitakavyoponyoka mkononi mwake.
2Kwa hiyo Dawidi akaondoka, akapita mpaka yeye na watu 600 waliokuwa naye, wakaenda kwa Akisi, mwana wa Maoki, mfalme wa Gati.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.