1Baada ya siku sita Yesu akamchukua Petero na Yakobo na Yohana nduguye, akapanda pamoja nao peke yao juu ya mlima mrefu.
2Huko akageuzwa sura yake machoni pao. Uso wake ukamulika kama jua, nazo nguo zake zikamerimeta kama mwanga.Kijana mwenye pepo.(14-21: Mar. 9:14-29; Luk. 9:37-42.)
14Walipofika penye kundi la watu, mtu akamjia, akampigia magoti, akasema:
15Bwana, umhurumie mwanangu! Kwani ni mwenye kifafa, aumia vibaya. Kwani mara nyingi huanguka motoni, tena mara nyingi huanguka majini.
16Nikampeleka kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.
17Yesu akajibu akisema: Enyi wa kizazi kisichomtegemea Mungu kwa kupotoka! Nitakuwapo nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa, nilipo!5 Mose 32:5; Yoh. 14:9.
18Yesu alipomkaripia, pepo akamtoka; naye mtoto akapona tangu saa ileile.
19Kisha wanafunzi wakamjia Yesu, alipokuwa peke yake, wakasema: Mbona sisi hatukuweza kumfukuza huyo?Mat. 10:1.
20Naye akawaambia: Ni kwa ajili hammtegemei Mungu vema. Maana nawaambia la kweli: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mlima huu: Ondoka hapa, ulipo, uende pale! nao utaondoka. Hivyo halitakuwako neno lisilowezekana nanyi.Mat. 21:21; Luk. 17:6; 1 Kor. 13:2.
21Lakini kabila hili la pepo halitoki isipokuwa kwa nguvu ya kuomba na ya kufunga.
Ufunuo wa pili wa mateso.(22-23: Mar. 9:30-32; Luk. 9:43-45.)22Walipokuwa wakizunguka huko Galilea, Yesu akawaambia: Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwa watu,
23nao watamwua, kisha siku ya tatu atafufuliwa. Wakasikitika sana.
Kodi ya Nyumba ya Mungu.24Walipofika Kapernaumu, watoza kodi wakamjia Petero, wakasema: Mfunzi wenu halipo kodi?2 Mose 30:13.
25Akasema: Hulipa. Naye alipokuja nyumbani, Yesu akaanza kumwuliza akisema: Waonaje, Simoni, wafalme wa nchi huwatoza watu gani chango au kodi? Wana wao wenyewe au wageni?
26Alipojibu: Huwatoza wageni, Yesu akamwambia: Basi, wana wenyewe hawatozwi.
27Lakini tusiwakwaze! Nenda pwani, uloe kwa ndoana! Kisha samaki wa kwanza atakayezuka umshike, ufumbue kinywa chake! Mle utaona fedha, itwae, ukawape kwa ajili yetu, mimi na wewe!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.