4 Mose 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Makambi yanateketea upande.

1Lakini watu wakanuna, vikawa vibaya masikioni mwa Bwana; naye Bwana alipovisikia, makali yake yakawaka moto, nao moto wa Bwana ukawawakia, ukayala makambi yaliyokuwa pembeni.Majibu ya Bwana.

16Bwana akamwambia Mose: Toa katika wazee wa Waisiraeli watu 70, uwakusanye kwangu, nao wawe watu, unaowajua, ya kuwa ndio wazee wa watu walio wenye amri, uwapeleke penye Hema la Mkutano, wajipange hapo pamoja na wewe.

23Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Je? Mkono wa Bwana umegeuka kuwa mfupi? Sasa utaona, kama neno langu linakupatia kitu, au kama ni la bure.Yes. 50:2; 59:1.

24Kisha Mose akatoka, akawaambia watu hayo maneno ya Bwana; akatoa katika wazee wa Waisiraeli watu 70, akawakusanya, akawapanga, walizunguke Hema.

25Ndipo, Bwana aliposhuka winguni kusema naye, nayo roho iliyomkalia akaichukua nusunusu, akawagawia hao wazee 70; ikawa, roho ilipotua juu yao, ndipo, walipofumbua mambo, lakini hawakuendelea.

26Kulikuwa na watu wawili waliosalia makambini, mmoja jina lake Eldadi, wa pili jina lake Medadi, nao roho ikatua juu yao, kwani walikuwa wameandikwa, lakini hawakutokea Hemani, nao wakafumbua mambo makambini.

27Ndipo, kijana alipopiga mbio kumpasha Mose habari kwamba: Eldadi na Medadi wamo makambini wakifumbua mambo.

28Yosua, mwana wa Nuni, aliyekuwa mtumishi wake Mose tangu ujana wake, akajibu na kusema: Bwana wangu Mose, wakomeshe!4 Mose 13:16; 2 Mose 24:13.

29lakini Mose akamwambia: Wewe unaona wivu kwa ajili yangu mimi? Laiti watu wote wa Bwana wangekuwa wafumbuaji, Bwana akiwagawia roho yake!Mar. 9:39; Yoe. 2:28.

30Kisha Mose akarudi tena makambini yeye pamoja na hao wazee wa Waisiraeli.

Watu wanapata nyama, wengi wanauawa na uchu.

31Ndipo, upepo ulipotoka kwake Bwana, ukatoa tombo upande wa baharini, ukawatawanya po pote penye makambi, kupita katikati yao ulikuwa mwendo wa siku moja upande wa huku, nao upande wa huko ulikuwa mwendo wa siku moja, vivyo hivyo kuyazunguka makambi yote, tena juu ya nchi ilikuwa mikono miwili kuupima wingi wao.2 Mose 16:13.

32Watu wakaondoka, wakawa wakiwaokota hao tombo mchana kutwa na usiku kucha, tena mchana wa kesho; aliyeokota machache aliokota frasila mia, wakawaanika pande zote za kuyazunguka makambi.

33Lakini nyama zilipokuwa zingaliko vinywani mwao, zilipokuwa hazijaisha kutafunwa, ndipo, makali ya Bwana yalipowawakia hao watu, naye Bwana akawapiga hao watu pigo kubwa mno.

34Kwa hiyo walipaita mahali pale Makaburi ya uchu, kwa kuwa walizika hapo watu waliouawa na Uchu mwingi.1 Kor. 10:6.

35Watu walipoondoka hapo penye Makaburi ya Uchu wakaenda Haseroti, wakakaa Haseroti.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help