Ezera 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Wayuda wanazuiliwa kuendelea kuijenga Nyumba ya Mungu.

1Wapingani wao Wayuda na Wabenyamini waliposikia, ya kuwa waliorudi kwenye kutekwa wanamjengea Bwana Mungu wa Isiraeli Jumba,

2ndipo, walipomkaribia Zerubabeli nao waliokuwa vichwa vya milango, wakawaambia: Na tujenge pamoja nanyi! Kwani nasi tunamtumikia Mungu wenu kama ninyi, tunamtambikia tangu hapo, Esari-Hadoni, mfalme wa Asuri, alipotuleta huku, tukae.

6Ahaswerosi alipoupata ufalme, katika siku za mwanzo wa ufalme wake wakaandika barua ya kuwashtaki waliokaa Yuda na Yerusalemu.

7Siku za Artasasta Bisilamu na Mitiridati na Tabeli na wenziwe wengine wakaandika barua kwa Artasasta, mfalme wa Wapersia; nayo maandiko ya barua hii yalikuwa yameandikwa Kishami, nayo maneno yake yalikuwa yamegeuzwa kuwa ya Kishami vilevile:

8Mwenye amri Rehumu na mwandishi Simusai waliandika barua moja kwa mfalme Artasasta kwa ajili ya Yerusalemu ya kwamba:

9Kale mwenye amri Rehumu na mwandishi Simusai na wenzao wengine waliandika barua, wao pamoja na Wadinai na Waafarsatiki, tena Watarpeli, Waafarsi, Waarkewi, Wababeli, Wasusaniki, Wadehai, Waelamu

10na makabila mengine, Osinapari aliyekuwa mwenye ukuu na utukufu aliowateka na kuwahamisha akiwakalisha katika miji ya Samaria na katika miji mingine iliyoko ng'ambo hii ya jito kubwa na penginepengine;

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help