1Yosefu asipoweza kuvumilia tena kwa ajili yao wote waliosimama kwake, ndipo alipoita kwamba: Watoeni wote humu mwangu! Kwa hiyo hakusimama mtu mwake, Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake.
2Lakini alipopaza sauti kwa kulia, Wamisri wakavisikia, nao wa nyumbani mwa Farao wakavisikia.
3Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Ni mimi Yosefu! Baba yangu yuko mzima bado? Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walimstukia.
4Ndipo, Yosefu alipowaambia ndugu zake: Nifikieni karibu! Nao walipokwisha kumkaribia, akawaambia: Ni mimi ndugu yenu Yosefu, mliyemwuza kupelekwa Misri.
25Ndivyo, walivyotoka Misri, wapande kwenda katika nchi ya Kanaani kwa baba yao Yakobo.
26Wakamsimulia kwamba: Yosefu yuko mzima bado, naye ndiye anayeitawala nchi yote nzima ya Misri; lakini moyo wake ukapigwa bumbuazi, hakuyategemea maneno yao.
27Wakamwambia maneno yote, Yosefu aliyowaambia; naye alipoyaona hayo magari, Yosefu aliyoyatuma kumchukua, ndipo, roho yake ilipomrudia baba yao Yakobo.
28Kisha Isiraeli akasema: Lililo kuu ni hili: mwanangu Yosefu angaliko mzima. Nitakwenda, nimwone, kabla sijafa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.