Iyobu 21 - Swahili Roehl Bible 1937

1Sikieni na kulisikiliza neno langu!

2Hili litakuwa la kuituliza mioyo yenu.

3Niacheni, nipate kusema mimi nami! Nitakapokwisha kuyasema yangu, na msimange tena.

4Je? Yuko mtu, ninayemsuta? Mbona sishindwi na kuvumilia?

5Nigeukieni mimi, mpate kustuka na kuiweka mikono vinywani mwenu!

6Kweli nami nikiyakumbuka nashikwa na woga, mwili wangu nao unakufa ganzi.

7Mbona wasiomcha Mungu huwapo? Mbona huwa wazee, nguvu zao zikiendelea kuongezeka?

17Taa zao wasiomcha Mungu zikizima, ni mara ngapi? Si kila mara, unapowajia mwangamizo wao? Ni mara ngapi, Mungu akiwapatia matanzi kwa kuwakasirikia,

27Tazameni! Ninayajua mawazo yenu nayo mashauri yenu ya kunikorofisha.

28Mwasema: Nyumba ya mkuu aliyetesa watu iko wapi? Mahema, wasiomcha Mungu waliomokaa, yako wapi nayo?

29Je? Wapitao njiani hamkuwauliza hayo? Hamzitambui habari zao za mambo, waliyoyaona wao?

30Kwamba: Siku ya msiba mbaya hupona, siku, makali yanapotokea, huepuka.

31Yuko nani anayeziumbua njia zake usoni pake? Tena yuko nani anayemlipisha aliyoyafanya yeye?

32Naye husindikizwa mpaka mazikoni, tena kaburini kwake wanangoja zamu.

33Udongo wa bondeni anauona kuwa mtamu, watu wote wanamfuata nyuma yake, nao waliomtangulia hawahesabiki.

34Nanyi mnaniambiaje matulizo ya moyo yaliyo ya bure? Kwani yanayosalia ya majibu yenu, ni ukatavu tu.

Elifazi anasema mara ya tatu: Iyobu hana budi kujuta.

Elifazi wa Temani akajibu akisema:

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help