1Mungu, umetutupa na kututapanya; kweli ulikuwa umetuchafukia, lakini utugeukie!(7-14: Sh. 108:7-14.)
5Kusudi wao uwapendao wapate kuopoka, mkono wako wa kuume uwaokoe, ukituitikia!
6Mungu alisema hapo Patakatifu pake: Nikiigawanya nchi ya Sikemu nitapiga vigelegele; ndipo, nitakapolipima nalo bonde la Sukoti.
7Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, Efuraimu ni kingio la kichwa changu, Yuda ni bakora yangu ya kifalme.1 Mose 49:10.
8Moabu ni bakuli langu la kunawia, Edomu ndiko, nitakakovitupia viatu vyangu, nchi ya Wafilisti itanishangilia.
9Yuko nani atakayenipeleka mjini mwenye maboma? Yuko nani atakayeniongoza mpaka Edomu?
10Si wewe Mungu uliyenitupa, ukakataa kwenda vitani na vikosi vyetu?
11Tujie, utusaidie, tumshinde atusongaye! Kwani watu hawawezi kutuokoa.
12Kwa nguvu yake Mungu na tufanye nasi yenye nguvu! Yeye ndiye atakayewakanyaga watusongao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.