1Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, akimchinja au akimwuza, kwa ng'ombe mmoja sharti alipe ng'ombe watano, na kwa kondoo mmoja sharti alipe kondoo wanne.
14Mtu akikopa nyama kwa mwenzake, naye huyo nyama akiumia au akifa, bwana wake akiwa hayuko, yule hana budi kumlipa.
15Kama bwana wake yuko hapo, halipi; kama alimkodisha huyo nyama, malipo yamo katika hizo fedha za kukodisha.
16Mtu akimdanganya mwanamwali asiyeposwa, alale naye, sharti amlipie mali za ukwe, awe mkewe.
19Kila atakayelala na nyama sharti auawe kabisa.
20Mtu atakayetambikia miungu mingine, isipokuwa Bwana peke yake, sharti atiwe mwiko wa kuwapo.
21Mgeni usimwonee wala usimkorofishe! Kwani nanyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
25Ukiwakopesha fedha watu wa ukoo wangu, wakikaa kwako wenye ukosefu, usiwawie kama wakopeshaji wengine, ni kwamba: Msiwatoze faida kubwa za kukopesha!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.