1*Niliwafurahia walioniambia: Twende Nyumbani kwa Bwana!Sh. 26:6-8.
2Hivyo miguu yetu iko ikisimama malangoni kwako, Yerusalemu.
3Yerusalemu umejengwa tena kama mji ulioungamanishwa vema.
4Ndiko, mashina ya watu yanakopanda, yaliyo mashina ya Bwana; ndiko, wanakowashuhudia Waisiraeli, walishukuru Jina la Bwana.
5Kwani viti vya uamuzi vilipowekwa, ndipo pale, ni viti vya kifalme vya mlango wa Dawidi.
6Uombeeni Yerusalemu utengemano, watengemane nao waupendao!Zak. 4:7.
7Sharti uwe utengemano ndani ya boma lako, nao utulivu katika majumba yako yaliyo mazuri mno.
8Kwa ajili yao walio ndugu zangu na rafiki zangu na niseme tena na kuomba: Utengemano na uwe kwako!
9Kwa ajili ya Nyumba ya Bwana Mungu wetu na nikutafutie mema.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.