4 Mose 22 - Swahili Roehl Bible 1937

Bileamu anaitwa, awaapize Waisiraeli.

1Wana wa Isiraeli walipoondoka huko wakapiga makambi kwenye mbuga za Moabu ng'ambo ya huku ya Yordani, Yeriko ukiwa ng'ambo ya pili.

2Balaka, mwana wa Sipori, alipoyaona yote, Waisiraeli waliyowafanyizia Waamori,

3Wamoabu wakaingiwa na woga mwingi sana wa hao watu kwa kuwa wengi sana, nao Wamoabu wakawastukia sana wana wa Isiraeli.

4Ndipo, Wamoabu walipowaambia wazee wa Wamidiani: Makundi hayo yatameza yote yanayotuzunguka, kama ng'ombe anavyomeza majani ya porini. Ndipo, Balaka, mwana wa Sipori, aliyekuwa mfalme wa Wamoabu siku zile

5alipotuma wajumbe kwenda Petori kwa Bileamu, mwana wa Beori, aliyekaa kwenye lile jito kubwa katika nchi yao walio ukoo wake, wamwite na kumwambia: Tazama, wako watu waliotoka Misri, nao wanaifunika nchi hii pote, unapotazama, tena wanakaa kunielekea mimi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help