3 Mose 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Ng'ombe za tambiko za weuo.

1Bwana akamwambia Mose kwamba:

2Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Mtu akikosea agizo lo lote la Bwana asilikosee kwa kusudi, akifanya yasiyofanywa, ingawa ayafanye mara moja tu, na afanye hivyo:

3Mtambikaji aliyepakwa mafuta akiwaponza watu hawa, wakore manza kwa ajili ya kukosa kwake, basi, kwa ajili ya hilo kosa lake, alilolikosa, na apeleke dume la ng'ombe aliye mwana bado, asiye na kilema, wa kumtolea Bwana kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.

4Huyo dume atakapomfikisha mbele ya Bwana pa kuliingilia Hema la Mkutano au aubandike mkono wake kichwani pake huyo dume, kisha amchinje huyo dume mbele ya Bwana.

5Naye mtambikaji aliyepakwa mafuta na atwae damu nyingine ya huyo dume na kuiingiza Hemani mwa Mkutano.

6Kisha mtambikaji na achovye kidole chake katika damu, anyunyize damu kidogo mara saba mbele ya Bwana penye lile pazia la kupakingia Patakatifu.

13Mkutano wote wa Waisiraeli wakikosa neno, isipokuwa kwa kusudi, nalo hilo neno halikujulikana machoni pao wote, ya kuwa wamelikosea agizo moja tu katika maagizo yote ya Bwana wakifanya yasiyofanywa, basi, kama wamekora manza hivyo,

22Mkuu wa watu atakapokosea agizo lo lote la Bwana Mungu wake na kufanya tendo moja tu lisilofanywa, kama hakulifanya kwa kusudi, basi, akikora manza hivyo,

23au hapo kosa lake, alilolikosa, litakapojulikana kwake kuwa ni kosa, na apeleke dume la mbuzi asiye na kilema kuwa toleo lake.

24Kisha na aubandike mkono wake kichwani pake huyo dume, kisha amchinje mahali hapo, wanapochinja mbele ya Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima; hivyo naye atakuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.

25Kisha mtambikaji na atwae damu nyingine ya huyu ng'ombe ya tambiko ya weuo kwa kidole chake, azipake pembe za meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, nayo damu yake nyingine aimwagie misingi ya meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko.

26Nayo mafuta yake yote na ayachome moto mezani pa kutambikia kama mafuta ya ng'ombe ya tambiko ya shukrani. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi, aondolewe kosa lake.

27Lakini mtu aliye mtumtu tu katika nchi hii akikosa, asipokosea agizo la Bwana kwa kusudi, akifanya tendo moja tu lisilofanywa, basi, akikora manza hivyo,

28au hapo kosa lake, alilolikosa, litakapojulikana kwake kuwa ni kosa, na apeleke jike la mbuzi asiye na kilema kuwa toleo lake kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa.

29Kisha na aubandike mkono wake kichwani pake huyo ng'ombe ya tambiko ya weuo, kisha amchinje huyo ng'ombe ya tambiko ya weuo mahali hapo, wanapochinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.

30Kisha mtambikaji na atwae damu yake nyingine kwa kidole chake, azipake pembe za meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, nayo damu yake nyingine yote aimwagie misingi ya meza ya kutambikia.

31Nayo mafuta yake yote na ayaondoe, kama mafuta yanavyoondolewa katika ng'ombe ya tambiko ya shukrani. Kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia, yawe mnuko wa kumpendeza Bwana. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi, aondolewe kosa lake.

32Lakini kama anapeleka kondoo, amtoe kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo sharti apeleke jike asiye na kilema.

33Kisha na aubandike mkono wake kichwani pake huyo ng'ombe ya tambiko ya weuo kisha amchinje huyo ng'ombe ya tambiko ya weuo mahali hapo, wanapochinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.

34Kisha mtambikaji na atwae damu nyingine ya huyo ng'ombe ya tambiko ya weuo kwa kidole chake, azipake pembe za meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko, nayo damu yake nyingine yote aimwagie misingi ya meza ya kutambikia.

35Nayo mafuta yake yote na ayaondoe, kama mafuta ya kondoo aliye ng'ombe ya tambiko ya shukrani yanavyoondolewa, kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia juu ya mioto ya Bwana. Ndivyo, mtambikaji atakavyompatia upozi, aondolewe kosa lake, alilolikosa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help