4 Mose 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Hesabu ya wapiga vita wa Kiisiraeli.

1Siku ya kwanza ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri Bwana akamwambia Mose katika nyika ya Sinai Hemani mwa Mkutano kwamba:

2Toeni jumla yao wote walio mkutano wa wana wa Isiraeli kwa ndugu zao na kwa milango ya baba zao, mkiyahesabu majina ya wana waume wote kichwa kwa kichwa.

3Kuanzia kwao wenye miaka ishirini na zaidi wewe na Haroni mwakague wote pia wanaoweza kwenda vitani kwao Waisiraeli, kikosi kwa kikosi.

4Tena mchukue kuwa nanyi kwa kila shina moja mtu mmoja aliye kichwa chao walio wa mlango wa baba yake.

5Nayo haya ndiyo majina yao, ninaowataka, wasimame pamoja nanyi: wa Rubeni Elisuri, mwana wa Sedeuri;

6wa Simeoni Selumieli, mwana wa Surisadai;

47Lakini Walawi hawakuhesabiwa katikati yao kwa hivyo, shina la baba zao lilivyokuwa.

Kutengwa kwao Walawi.

48Bwana akamwambia Mose kwamba:

49Wao wa shina la Lawi usiwakague, wala jumla yao usiitie katika hiyo ya wana wa Isiraeli.4 Mose 2:33; 3:15.

50Ila utawaweka Walawi kuliangalia Kao l Ushahidi na vyombo vyake vyote nayo yote yaliyomo. Wao ndio watakaolichukua kao na vyombo vyake vyote, nao ndio watakaolitumikia, nao wakipiga makambi yao, hayo na yalizunguke.4 Mose 3:23-38; 4.

51Kao litakapoondoka, wao Walawi ndio watakaolishusha chini; tena Kao litakapofika makambini, Walawi ndio watakaolisimamisha; lakini mgeni atakayelikaribia hana budi kuuawa.

52Wana wa Isiraeli watakapopiga makambi, kila mtu na apige hema katika kambi lake penye bendera ya kikosi cha kwao.

53Lakini Walawi na wapige makambi kulizunguka Kao la Ushahidi, makali yangu yasiwajie wao wa mkutano wa wana wa Isiraeli; kwa hiyo Walawi na wangoje zamu ya kuliangalia Kao la Ushahidi.

54Wana wa Isiraeli wakayafanya yote; kama Bwana alivyomwagiza Mose, ndivyo, walivyofanya kuwa sawasawa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help