2 Mose 8 - Swahili Roehl Bible 1937

Pigo la pili: Vyura wengi.

1Kisha Bwana akamwambia Mose: Nenda kwa Farao, umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!

8Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Niombeeni kwa Bwana, awaondoe hawa vyura kwangu na kwa watu wangu! Ndipo, nitakapowapa ruhusa watu wa ukoo huu kwenda zao, wamtambikie Bwana.Pigo la tatu: Mbu wengi.

16Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Inyanyue fimbo yako, uyapige mavumbi ya chini, yageuke kuwa mbu katika nchi yote ya Misri!

17Wakafanya hivyo; Haroni alipoukunjua mkono wake wenye fimbo yake na kuyapiga mavumbi ya chini, yakageuka kuwa mbu, wakawauma watu na nyama; mavumbi yote ya nchi yakageuka kuwa mbu katika nchi yote ya Misri.

18Waganga nao walipofanya hivyo, watokeze mbu kwa uganga wao, hawakuweza; nao wale mbu wakawauma watu na nyama.Pigo la nne: Mainzi wabaya.

20Bwana akamwambia Mose: Kesho asubuhi na mapema ujidamke, upate kumtokea Farao, utakapomwona, akitoka kwenda majini! Ndipo umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help