5 Mose 22 - Swahili Roehl Bible 1937

Maagizo mengine ya kupenda watu na nyama na mengine.

1Utakapoona, ng'ombe au kondoo wa ndugu yako wakipotea, usijifiche kuwa kama mtu asiyewaona, ila sharti uwarudishe kwake ndugu yako.

8Utakapojenga nyumba mpya, sharti juu darini utengeneze kikingio, usifanye nyumbani mwako kuwa mwenye damu ya mtu, mtu akianguka huko.

9Shamba lako la mizabibu usilipande mbegu za namna mbili, lote pia lisiwe mali ya Patakatifu: mbegu, ulizozipanda, pamoja na mazao ya mizabibu.

12Jifanyizie vishada penye pembe zote nne za nguo zako za kijifunika!Mapatilizo ya ugoni.

13Itakuwa, mtu amwoe mkewe na kuingia kwake, kisha achukizwe naye.

14Kwa hiyo atamsingizia mambo ya uwongo, ampatie jina baya na kusema: Nimemwoa mwanamke huyu; lakini nilipoingia kwake sikumwona kuwa mwanamwali.

15Vitakapokuwa hivyo, babake na mamake yule msichana na wamchukue na kumpeleka kwa wazee wa mji huo langoni pake pamoja nayo yanayoweza kuujulisha uwanawali wake.

16Naye babake yule msichana na awaambie wazee: Nimempa mwanangu mtu huyu kuwa mkewe, kisha akachukizwa naye;

17akamsingizia mambo ya uwongo kwamba: Sikumwona kuwa mwanamwali. Lakini yatazameni haya yanayoujulisha uwanawali wa mwanangu! Kisha waikunjue hiyo nguo mbele ya wazee wa mji huo.

18Kwa hiyo wazee wa mji huo na wamchukue yule mwanamume, wamchape.

19Kisha wamtoze fedha mia, wampe babake msichana, kwa kuwa yule alimpatia msichana wa Kiisiraeli jina baya; kisha awe mkewe, asiweze kumpa ruhusa kwenda zake siku zake zote.

20Lakini lile neno likiwa la kweli, nayo yanayoujulisha uwanawali wake yasipoonekana,

21na wampeleke yule msichana hapo pa kuiingilia nyumba ya baba yake, hapo watu wa mji wote wampige mawe, hata afe, kwa kuwa alifanya ujinga mbaya kwao Waisiraeli wa kufanya ugoni nyumbani mwa baba yake. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.

22Mtu atakapooneka, ya kuwa amelala na mwanamke aliyeolewa na mwingine, sharti wafe wote wawili, yule mwanamume aliyelala na mwanamke, naye mwanamke. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo kwao Waisiraeli.

23Mwanamwali akiisha kuposwa na mtu, tena mwingine aliyemkuta mjini akilala naye,

24sharti mwapeleke wote wawili langoni pa mji huo, mwapige mawe, hata wafe, yule kijana wa kike, kwa kuwa hakupiga kelele mjini, naye yule mwanamume, kwa kuwa amemkorofisha mchumba wa mwenzake. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.

25Lakini mwanamume atakapomkuta shambani kijana wa kike aliyekwisha kuposwa, akamkamata kwa nguvu, akalala naye, basi, huyu mwanamume aliyelala naye atakufa peke yake,

26lakini yule kijana wa kike msimfanyizie neno, kwani yule kijana wa kike hakukosa neno lipasalo, auawe, kwa kuwa jambo hili ni sawasawa, kama mtu aliyemwinukia mwenziwe na kumwua, afe.

27Kwani alimkuta shambani, naye yule kijana wa kike aliyekwisha kuposwa alipolia, hakuwako aliyemwokoa.

28Mtu atakapoona mwanamwali asiyeposwa bado, akamshika na kulala naye, basi, wakionwa,

29yule mwanamume aliyelala naye sharti ampe babake yule kijana wa kike fedha hamsini, kisha sharti awe mkewe, kwa kuwa amemkorofisha, naye hana ruhusa kumwacha siku zake zote.

30Mtu asimchukue mkewe baba yake, wala asiifunue pembe ya nguo zake!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help