1Ndipo, mfalme Dario alipotoa amri, wakachunguza nyumbani mwenye vitabu, mlimowekwa navyo vilimbiko vya huko Babeli.
2Kisha kikaoneka kizingo cha karatasi katika mji wa Ahimeta katika nchi ya Media; ndimo, nalo jumba la mfalme lilimokuwa. Ile karatasi ilikuwa imeandikwa: Ukumbusho.
3Kwamba: Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Kiro huyu mfalme Kiro akatoa amri, Nyumba ya Mungu huko Yerusalemu na ijengwe kuwa mahali, watakapotoa ng'ombe za tambiko, misingi yake itengenezwe kuwa na nguvu; urefu wake uwe mikono sitini, nao upana wake uwe mikono sitini.Sikukuu ya Pasaka.
19Kisha wao waliotoka kwenye kutekwa wakafanya sikukuu ya Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.2 Mose 12:6.
20Kwani watambikaji na Walawi walijitakasa pamoja, wakatakata wote pia, wakawachinjia kondoo wa Pasaka wote waliotoka kwenye kutekwa nao ndugu zao watambikaji nao wao wenyewe.
21Wana wa Isiraeli waliorudi kwenye kutekwa wakaila pamoja nao waliotaka kumfuata Bwana Mungu wa Isiraeli, waliojitenga, wasijichafue kwa wamizimu wenzao waliokaa kwao katika nchi hii.
22Wakaifanya hiyo sikukuu ya Mikate isiyochachwa siku saba na kufurahi, kwani Bwana aliwafurahisha kwa kuugeuza moyo wa mfalme wa Asuri, uwaelekee, aishupaze mikono yao katika kazi ya Nyumba ya Mungu aliye Mungu wa Isiraeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.