5 Mose 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Matendo makuu, Mungu aliyowafanyizia Waisiraeli.

1Kwa hiyo umpende Bwana Mungu wako na kuyaangalia mambo yake yanayopasa, uyaangalie siku zote, maongozi yake na maamuzi yake na maagizo yake!

2Ndipo, mtakapomtambua na leo; kwani sisemi na wana wenu, maana hawayajui, wala hawakuyaona mapatilizo ya Bwana Mungu wenu na matendo yake makuu na nguvu za kiganja chake na uwezo wa mkono wake, alipoukunjua.

3na vielekezo vyake na matendo yake yote, aliyomfanyizia Farao, mfalme wa Misri, nao wenyeji wa nchi yake kule kwao Misri,

4nayo aliyovifanyia vikosi vya Farao na farasi wake na magari yake, aliowafurikishia maji ya Bahari Nyekundu ya kuwatosa, walipokimbia, wawafikilie ninyi, Bwana akawaangamiza, wasionekane tena hata leo.Waisiraeli wanawekewa mbaraka na kiapizo.

18Kwa hiyo haya maneno yangu yawekeni mioyoni na rohoni mwenu! Tena yafungeni mikononi penu kuwa kielekezo, yawe napo mapajini penu katikati ya macho yenu!5 Mose 6:6-9.

19Yafundisheni watoto wenu na kuyasema nao ukikaa nyumbani mwako, ukienda safari zako, ukitaka kulala, hata ukiamka!

20Yaandike vizingitini namo milangoni nyumbani mwako!

21Ndipo, siku zenu nazo siku za wana wenu zitakapokuwa nyingi katika hiyo nchi, Bwana Mungu wenu aliyowaapia baba zenu kuwapa, iwe yao siku zote, mbingu zitakazokuwa juu ya nchi.

22Kwani mtakapoyaangalia vema haya maagizo yote, mimi ninayowaagiza ninyi, myafanye na kumpeda Bwana Mungu wenu na kuzishika njia zake na kugandamana naye,

23ndipo, Bwana atakapoyafukuza hayo mataifa yote mbele yenu, mchukue nchi za mataifa walio wengi na wenye nguvu kuliko ninyi.5 Mose 7:1-2.

24Ndipo, mahali po pote, nyayo za miguu yenu zitakapopakanyaga, patakapokuwa penu, mpaka wenu utoke nyikani na Libanoni nako kwenye lile jito kubwa la Furati, ufike kwenye bahari ya machweoni kwa jua.

25Hatakuwako mtu atakayeweza kusimama mbele yenu, kwani Bwana Mungu wenu atawastusha, wawaogope ninyi katika nchi zote, mtakazozikanyaga, kama alivyowaambia ninyi.

26Tazameni, leo hivi mimi ninaweka mbele yenu mbaraka na kiapizo:5 Mose 30:1,15.

27mbaraka mtaipata mtakapoyasikia maagizo ya Bwana Mungu wenu, mimi ninayowaagiza leo.5 Mose 28:2,15.

28Lakini kiapizo kitawapata, msipoyasikia maagizo ya Bwana Mungu wenu, mwondoke katika njia hiyo, mimi ninayowaagiza leo, mkafuata miungu mingine, msiyoijua.

29Hapo, Bwana Mungu wako atakapokuingiza katika nchi hiyo, wewe utakayoiingia kuichukua, iwe yako, ndipo utoe mbaraka juu ya mlima wa Gerizimu, nacho kiapizo juu ya mlima wa Ebali5 Mose 27:12-13; Yos. 8:33-34.

30Milima hii iko ng'ambo ya huko ya Yordani nyuma ya njia inayokwenda machweoni kwa jua katika nchi ya Wakanaani wanaokaa katika nyika inayoelekea Gilgali, ni huko kando ya kimwitu cha More.1 Mose 12:6.

31Kwani ninyi mtauvukia Yordani kuichukua hiyo nchi, iwe yenu, Bwana Mungu wenu atakayowapa, nanyi mtaichukua, iwe yenu kweli, kisha mtaikaa.

32Kwa hiyo angalieni, myafanye haya maongozi na maamuzi yote, mimi ninayoyaweka leo mbele yenu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help