Ufunuo 13 - Swahili Roehl Bible 1937
Nyama mwenye pembe kumi na vichwa saba.
1Nikaona nyama mkali, akitoka baharini mwenye pembe kumi na vichwa saba; juu hizo pembe zake zilikuwa na vilemba kumi vya kifalme, napo vichwani pake palikuwa na majina ya kumtukana Mungu.