Yosua 24 - Swahili Roehl Bible 1937

Yosua anawaaga Waisiraeli.

1Kisha Yosua akayakusanya mashina yote ya Waisiraeli huko Sikemu, akawaita wazee wa Waisiraeli na wakuu wao na waamuzi wao na wenye amri wa kwao, wakajipanga mbele ya Mungu.

2Ndipo, Yosua alipowaambia watu wote: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wenu anavyosema: Tangu kale baba zenu, walipokaa ng'ambo ya huko ya lile jito kubwa, naye Tera, babake Aburahamu na babake Nahori, walitumikia miungu mingine.

16Ndipo, watu walipojibu wakisema: Shauri hili na litukalie mbali la kumwacha Bwana na kutumikia miungu mingine.

17Kwani Bwana ni Mungu wetu. Yeye ndiye aliyetuleta huku na kututoa sisi na baba zetu katika nchi ya Misri nyumbani, tulimokuwa watumwa, naye ndiye aliyevifanya vile vielekezo vikubwa machoni petu, naye alituangalia katika njia zote, tulizokwenda, na katika makabila yote, ambao tulipita katika nchi zao.

18Yeye Bwana ndiye aliyeyafukuza makabila yote machoni petu, nao Waamori waliokuwa wenyeji wa nchi hii; kwa hiyo nasi tutamtumikia Bwana, kwani yeye ni Mungu wetu.

19Naye Yosua akawaambia watu: Hamwezi kumtumikia Bwana, kwani yeye ni Mungu mtakatifu, tena Mungu mwenye wivu, kwa hiyo hatayavumilia mapotovu yenu na makosa yenu.2 Mose 20:5; 5 Mose 5:29.

20Kwani mtakapomwacha Bwana na kutumikia miungu migeni, atawafanyizia mabaya tena, awamalize ninyi akiacha kuwafanyizia mema.

21Lakini watu wakamwambia Yosua: Hivi havitakuwa, kwani tutamtumikia Bwana.

22Ndipo, Yosua alipowaambia watu: Ninyi mnajishuhudia wenyewe, ya kuwa mmejichagulia kumtumikia Bwana; nao wakaitikia kwamba: Tunajishuhudia hivyo.

23Naye akasema: Sasa iondoeni miungu hiyo migeni iliyoko kwenu! Kisha ielekezeni mioyo yenu kumtazamia Bwana Mungu wa Isiraeli!1 Mose 35:2.

24Ndipo, watu walipomwambia Yosua: Bwana Mungu wetu ndiye, tutakayemtumikia na kuisikia sauti yake.

25Ndivyo, Yosua alivyoagana na watu siku hiyo akiwatolea maongozi na maamuzi huko Sikemu.2 Fal. 23:3.

26Kisha Yosua akayaandika haya mambo yote katika kitabu cha Maonyo ya Mungu, akachukua jiwe kubwa, akalisimika chini ya mkwaju uliokuwako huko kwenye Patakatifu pa Bwana.1 Mose 35:4; Amu. 9:6.

27Kisha Yosua akawaambia watu wote: Tazameni! Jiwe hili na lituwie shahidi! Kwani limeyasikia maaneno yote, Bwana aliyoyasema na sisi. Kwa hiyo litakuwa shahidi lenu, msimwongopee Mungu wenu!1 Mose 31:48; Yos. 22:27.

28Kisha Yosua akawapa watu ruhusa kwenda kwao kila mtu kwenye fungu lake.

Kufa kwao Yosua na Elazari na kuizika mifupa yake Yosefu.

29Ikawa, hayo yalipomalizika, akafa Yosua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, mwenye miaka 110.

30Wakamzika katika mipaka ya fungu lake huko Timunati-Sera ulioko mlimani kwa Efuraimu upande wa kaskazini wa mlima wa Gasi.Yos. 19:50.

31Nao Waisiraeli wakamtumikia Bwana siku zote, Yosua alizokuwapo, nazo siku zote, walizokuwapo wale wazee waliokaa siku nyingi kuliko Yosua, ndio wale walioyajua yale matendo yote, Bwana aliyowatendea Waisiraeli.Amu. 2:7.

32Nayo mifupa ya Yosefu, wana wa Isiraeli waliyokuja nayo walipotoka Misri, wakaizika Sikemu katika fungu lile la shamba, Yakobo alilolinunua kwa vipande mia vya fedha kwa wana wa Hamori, babake Sikemu; kwa hiyo hilo fungu likawa lao wana wa Yosefu.1 Mose 33:19; 50:25.

33Elazari, mwana wa Haroni, alipokufa, wakamzika huko Gibea uliokuwa mji wa mwanawe Pinehasi, maana ndio, aliogawiwa milimani kwa Efuraimu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help