2 Mambo 15 - Swahili Roehl Bible 1937

Mfumbuaji Azaria anamshikiza Asa.

1Roho ya Mungu ikaja kumkalia Azaria, mwana wa Odedi,

2akamtokea Asa, akamwambia: Nisikilizeni, wewe Asa nanyi nyote Wayuda na Wabenyamini: Bwana yuko pamoja nanyi, mkiwa naye; mkimtafuta, atawaonekea ninyi, lakini mkimwacha, atawaacha nanyi.

3Siku nyingi Waisiraeli walikuwa pasipo Mungu wa kweli, pasipo mtambikaji aliyewafundisha Maonyo.Sikukuu ya kumshukuru Mungu.

8Asa alipoyasikia hayo maneno ya ufumbuaji wa mfumbuaji Odedi akajishupaza, akayatowesha matapisho katika nchi yote ya Yuda na ya Benyamini, hata katika miji, aliyoiteka milimani kwa Efuraimu, nayo meza ya kumtambikia Bwana iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Bwana akairudishia upya.

9Kisha akawakusanya Wayuda na Wabenyamini wote nao waliokaa ugenini kwake, Waefuraimu na Wamanase na Wasimeoni, kwani wengi waliokuwa Waisiraeli walirudi upande wake walipoona, ya kuwa Bwana Mungu wake yuko pamoja naye.

10Wakakusanyika Yerusalemu katika mwezi wa tatu wa mwaka wa kumi na tano wa Ufalme wa Asa,

11wakamtolea Bwana siku hiyo ng'ombe za tambiko, walizozitoa katika mateka: ng'ombe 700 na kondoo 7000.

12Wakaagana, wamtafute Bwana Mungu wa baba zao kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote,(16-18: 1 Fal. 15:13-15.)

16Mfalme Asa akamwondoa naye mama yake Maka katika ukuu wake, kwa kuwa alitengeneza kinyago cha Ashera, nacho kinyago chake Asa akakikatakata na kukipondaponda, kisha akakiteketeza penye kijito cha Kidoroni.

17Lakini matambiko ya vilimani hayakutoweka kwao Waisiraeli, lakini moyo wake Asa ulikuwa mtimilifu siku zake zote.

18Navyo, baba yake alivyovitakasa, pamoja navyo alivyovitakasa mwenyewe, fedha na dhahabu na vyombo, akavipeleka Nyumbani mwa Mungu.

19Vita havikuwako hata mwaka wa 35 wa ufalme wa Asa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help