1Kwa hiyo Iyobu, yasikilize nitakayoyasema! Maneno yangu yote yategee masikio yako!
2Tazama! Nitakifumbua kinywa changu, ulimi wangu useme kinywani mwangu.
3Maneno yangu yananyoka kama moyo wangu; midomo yangu itayasema ninayoyajua, yaliyo ya kweli.
4Roho ya Mungu aliyeniumba na pumzi ya Mwenyezi zinanipa kuwapo.
5Kama utaweza na unijibu! Jiweke tayari kusimama usoni pangu!
6Tazama! Mimi na wewe kwake Mungu tu sawa, mimi nami nilifinyangwa kwa udongo.
29Tazama! Hayo yote ndiyo, Mungu anayoyafanya mara mbili, hata mara tatu,
30airudishe roho ya mtu, isitumbukie shimoni, mwanga wenye uzima umwangazikie.Sh. 56:13; 103:4.
31Tega masikio, Iyobu, unisikilize! Nyamaza tu, mimi niseme!
32Kama unaona la kusema, nijibu! Sema! Kwani nitapendezwa kukuona kuwa mwenye wongofu.
33Kama wewe huna la kusema, nisikilize! Nyamaza tu, nikufunze werevu ulio wa kweli!
Elihu anasema mara ya pili: Mungu hayapotoi yaliyo sawa.Elihu akajibu tena akisema:
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.