Yohana 13 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuwaosha miguu.

1*Sikukuu ya Pasaka ilipokuwa haijatimia, Yesu alikuwa amejua, ya kuwa saa yake imefika, autoke ulimwengu huu, aende kwa Baba; kwa kuwa aliwapenda watu wake waliomo ulimwenguni, akawapenda mpaka mwisho.

2Walipokula chakula cha jioni, Msengenyaji alikuwa amekwisha kutia moyoni mwa Yuda wa Simoni Iskariota mawazo ya kumchongea.Chakula cha Pasaka.

12Alipokwisha kuwaosha miguu akayatwaa mavazi yake, akakaa tena chakulani, akawaambia; Mwakitambua, nilichowafanyia?

13Ninyi mnaniita Mfunzi na Bwana, mnasema vema hivyo, kwani ndimi.Kumjulisha Yuda.(21-30: Mat. 26:21-25; Mar. 14:18-21; Luk. 22:21-23.)

21Yesu alipokwisha kuyasema haya akazizimka jrohoni, akawashuhudia akisema: Kweli kweli nawaambiani: Mwenzenu mmoja atanichongea.Yoh. 12:27.

22Wanafunzi wakatazamana, maana hawakumjua, aliyemsema.

23Palikuwapo mwanafunzi wake mmoja aliyeegamia kifuani pa Yesu, ndiye, Yesu aliyempenda.Yoh. 19:26; 20:2; 21:20.

24Simoni Petero akamkonyeza huyo, amwulize, kama ni nani, anayemsema.

25Kisha yule aliyemwegamia Yesu kifuani akamwuliza: Bwana, ni nani?

26Yesu akajibu: Ni yule, mimi nitakayemtowelea kitonge na kumpa. Basi, akatowelea kitonge, akakitwaa, akampa Yuda wa Simoni Iskariota.

27Alipokwisha kukila kile kitonge, ndipo, Satani alipomwingia. Yesu akamwambia: Utakachokifanya, kifanye upesi!Yoh. 13:2; Luk. 22:3.

28Lakini wale waliokaa chakulani hakuna aliyeitambua sababu ya kumwambia hivyo;

29wengine wakawaza: kwa sababu Yuda aliushika mfuko wa senti, Yesu alimwambia: Nunua chakula cha siku za sikukuu! au agawie maskini kidogo.Yoh. 12:6.

30Basi, yeye alipokwisha kukipokea kile kitonge akatoka nje papo hapo, lakini ulikuwa usiku.

Agizo jipya.

31*Yule alipokwisha toka, Yesu akasema: Sasa Mwana wa mtu ametukuzwa, naye Mungu ndiye aliyetukuzwa kwake.Yoh. 12:28.

32Kama Mungu alitukuzwa kwake, yeye Mungu atamtukuza kwake mwenyewe, tena atamtukuza upesi.Yoh. 12:23; 17:1-5.

33Vitoto, nipo pamoja nanyi bado kidogo; kisha mtanitafuta, lakini kama nilivyowaambia Wayuda: Ninyi hamwezi kupafika pale, ninapokwenda mimi, ndivyo, ninavyowaambia hata ninyi sasa.Yoh. 8:21.

34Nawapa agizo jipya: Mpendane! Kama nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo!Yoh. 15:12-13,17.

35Kwa hiyo wote watatambua, ya kama m wanafunzi wangu mimi, mtakapopendana ninyi kwa ninyi.*

Kumwonya Petero(36-38: Mat. 26:33-35; Mar. 14:29-31; Luk. 22:31-34.)

36Simoni Petero akamwambia: Bwana, unakwenda wapi? Yesu akajibu: Pale ninapokwenda, huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata halafu.Yoh. 7:34; 21:18-19.

37Petero akamwambia: Bwana, kwa nini siwezi sasa kufuatana na wewe?

38Hata roho yangu nitaitoa kwa ajili yako wewe.Mat. 26:34.

39Yesu akajibu: Uitoe roho yako kwa ajili yangu mimi? Kweli kweli nakuambia: Jogoo hatawika, usipokuwa umekwisha kunikana mara tatu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help