4 Mose 18 - Swahili Roehl Bible 1937

Kazi za watambikaji na za Walawi.

1Bwana akamwambia Haroni: Wewe na wanao na mlango wa baba yako pamoja na wewe mtatwikwa maovu yatakayoonekana Patakatifu; tena wewe pamoja na wanao mtatwikwa maovu ya utambikaji wenu.Matunzo ya watambikaji.

8Bwana akamwambia Haroni: Tazama, mimi nimekupa kuviangalia vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa, ninavyotolewa; kwa hiyo ninakupa vipaji vitakatifu vyote, wana wa Isiraeli wanavyovitoa, kuwa ujira wako wewe na wa wanao wa kupakwa mafuta. Hii na iwe haki yenu ya kale na kale.Mafungu ya kumi ni yao Walawi.

21Tena tazama: Wana wa Lawi ninawapa mafungu ya kumi yote yatakayotolewa nao Waisiraeli kuwa fungu lao, ni ujira wa utumishi wao wa kufanya kazi za utumishi wa Hema la Mkutano.3 Mose 27:30.

22Lakini tangu sasa wana wa Isiraeli wasilifikie tena Hema la Mkutano karibu, wasijikoseshe, wakajipatia kufa.

23Ila Walawi tu na wazifanye kazi za utumishi wa Hema la Mkutano, nao ndio watakaotwikwa manza, watakazozikora. Haya sharti yawe maongozi ya kale na kale ya kuviongoza vizazi vyenu, nanyi hamtapata fungu la nchi kuwa lenu katikati ya wana wa Isiraeli.

24Kwani ninawapa Walawi mafungu ya kumi, wana wa Isiraeli watakayoyatoa kuwa vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana; haya ninawapa Walawi kuwa fungu lao, kwa hiyo ninawaambia: Hamtapata fungu la nchi kuwa lenu katikati ya wana wa Isiraeli.

Mafungu ya kumi ya Walawi ni yao watambikaji.

25Bwana akamwambia Mose kwamba:

26Sema nao Walawi, uwaambie: Mtakapoyachukua mafungu ya kumi kwao wana wa Isiraeli, niliyowapa ninyi kuwa fungu lenu kwao, nanyi sharti mtoe humo vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana, navyo sharti viwe fungu la kumi la hayo mafungu ya kumi.

27Navyo hivyo vpaji vyenu vya tambiko vitawaziwa kuwa ngano zenu za mapurio yenu au mafuriko ya makamulio yenu.

28Nanyi mtakapovitoa hivyo vipaji vya tambiko vya kumnyanyulia Bwana vya mafungu yenu ya kumi, mtakayoyachukua kwa wana wa Isiraeli, sharti m mpe mtambikaji Haroni hivyo vipaji vya tambiko, mtakavyovitoa kwenu vya kumnyanyulia Bwana.

29Katika vipaji vyote, mtakavyopewa, sharti mtoe vipaji vya tambiko vyote viwapasavyo kuvitoa vya kumnyanyulia Bwana, nanyi sharti mtoe vile vitakavyokuwa vizuri zaidi vinavyopasa kutolewa humo kuwa vipaji vitakatifu.

30Kwa hiyo uwaambie: Mtakapotoa humo vilivyo vizuri zaidi kuwa vipaji vyenu vya tambiko vya kunyanyuliwa, vitawaziwa kuwa mapato ya Walawi ya mapurio yao na mapato ya makamulio yao.

31Nanyi na mvile mahali po pote ninyi nao walio wa milango yenu, kwani ni mishahara yenu ya utumishi wenu wa Hema la Mkutano.Mat. 10:10.

32Mtakapovitoa vilivyo vizuri zaidi katika mapato yenu kuwa vipaji vya tambiko, basi, hamtajikosesha kwa ajili yao, wala hamtavichafua vipaji vitakatifu vya wana wa Isiraeli, msife.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help