1Nilifanya agano na macho yangu, kisha ningewezaje kumtazama mwanamwali kwa kumtamani?
5Kama nilifanya mwenendo ulio wa uwongo, miguu yangu ikakimbilia yaliyo madanganyifu,
6Mungu na anipime kwa mizani iliyo sawa; ndipo, atakapojua, ya kuwa sikukosa.
7Kama nyayo zangu ziliiacha njia yake, kama moyo wangu ulizifuata tamaa za macho yangu, kama uchafu wo wote uligandamana na mikono yangu:
16Wanyonge niliwanyima walichokitaka kwangu? Au nilizimisha macho yaliyokuwa ya mjane?
24Kama nilitumia dhahabu kuwa egemeo langu, na kuziwazia zile dhahabu safi kuwa kimbilio langu,
31Walioingia hemani mwangu hawasemi: Yuko mtu asiyeshibishwa na nyama, alizompa?
32Kweli kwangu hakuwako mgeni aliyelala nje, mimi humfungulia mpitaji milango yangu.1 Mose 19:2; Ebr. 13:2.
33Je? Niliyafunika mapotovu yangu kama watu wengine? Au nilizificha manza, nilizozikora, kifuani pangu?
34Je? Pako, nilipoogopa wingi wa watu? Au yalinistusha mazomeo ya milango yao, hata nikanyamaza, nisitoke nyumbani?
35Kama ningepata mtu atakayenisikiliza, ningemwonyesha maandiko yangu, Mwenyezi anijibu. Kiko nacho kitabu, alichokiandika mwenye kunigombeza;Iy. 23:3-7.
36kweli hicho ningekichukua begani pangu, au ningekifunga kichwani pangu kuwa kilemba changu.
37Ningemsimulia hesabu ya nyayo zangu, tena ningekuwa kama mkuu wa watu, nimkaribie.
38Kama shamba langu linanisuta na kupiga kelele, kama matuta yake yanaitikia na kulia,
39kama niliyala mazao yake pasipo kulipa na kuizimisha roho yake mwenye shamba,Iy. 24:11.
40basi, penye ngano na patokee mangugi matupu, napo penye mawele ndago tu! Maneno, Iyobu aliyoyasema, yamekwisha.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.