Luka 16 - Swahili Roehl Bible 1937

Mtunza mali mpotovu.

1*Akawaambia wanafunzi wake: Kulikuwako mtu mwenye mali aliyekuwa na mtunza mali. Huyu aliposengenywa kwake, ya kuwa anatapanya mali zake,

2akamwita, akamwambia: Hayo nayasikiaje kwako? Toa hesabu ya utunzaji wako wa mali zangu! Kwani huwezi tena kuzitunza mali zangu.

3Mtunza mali akasema moyoni mwake: Nifanyeje? Kwani bwana wangu ananiondoa katika utunzaji wa mali. Kulima siwezi; nako kuomba, naona soni.

4Nimetambua, nitakavyofanya, kusudi wanipokee nyumbani mwao, nitakapoondolewa katika utunzaji wa mali.

5Akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja, akamwambia wa kwanza: Una deni gani kwa bwana wangu?

6Aliposema: Matanaki 100 ya mafuta, akamwambia: Kichukue cheti chako, ukae, uandike 50!

7Kisha akamwambia mwingine: Na wewe una deni gani? Naye aliposema: Makanda 100 ya mchele, akamwambia: Kichukue cheti chako, uandike 80!

8Naye bwana akamsifu yule mtunza mali mpotovu, ya kuwa alifanya werevu. Kwani wana wa dunia hii huwaendea wa kizazi chao wenye werevu kuliko wana wa mwanga.

14Mafariseo waliopenda fedha walipoyasikia hayo yote, wakamfyoza.Mwenye mali na Lazaro.

19*Kulikuwa na mtu mwenye mali aliyevaa nguo za kifalme na za hariri, tena kila siku hula vya urembo vilivyo vizuri sana.

20Kulikuwako hata maskini, jina lake Lazaro, alikuwa amewekwa mlangoni pake kwa kuwa mwenye vidonda.

21Akataka sana kushibishwa na makombo yaliyoanguka mezani pake mwenye mali; mbwa nao huja kumlamba vidonda vyake.

22Ikawa, maskini alipokufa akachukuliwa na malaika, akapelekwa kifuani pa Aburahamu. Kisha mwenye mali akafa naye, akazikwa.

23Alipokuwa kuzimuni katika maumivu akayainua macho yake, akamwona Aburahamu, yuko mbali, naye Lazaro alikuwa amekaa kifuani pake.

24Akaita akisema: Baba Aburahamu, nihurumie! Umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, aje, aupoze ulimi wangu! kwani naumia humu motoni.

25Aburahamu akasema: Mwanangu, kumbuka, ya kuwa uliyapokea mema yako katika maisha yako! Lakini Lazaro huko alipata maovu tu. Lakini sasa yeye anatulizwa moyo hapa, nawe wewe unaumia.

26Tena si kwa ajili hii tu, ila kati yetu sisi nanyi pameatuka ufa mkubwa, kusudi wanaotaka kupita toka hapa, wafike kwenu, wasiweze, wala toka huko wasiweze kupapita, wafike kwetu.

27Ndipo, alipojibu: Nakuomba, baba, umtume, aende nyumbani kwa baba yangu.

28Kwani ninao ndugu watano; aje, awashuhudie mambo ya hapa, nao wasije hapa penye maumivu.

29Aburahamu aliposema: Wanao Mose na Wafumbuaji, na wawasikilize wao!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help