1Bwana, unanichunguza, unanijua.
13Kwani wewe ndiwe uliyeyaumba mafigo yangu, ndiwe uliyeniunga tumboni mwa mama.
14Ninakushukuru, kwani ni ajabu litishalo, jinsi nilivyotengenezwa, vilivyo kazi zako hustaajabisha kweli, roho yangu inavijua sanasana.
15Mifupa yangu haikuwa imefichika, usiione, nilipofanyiziwa mahali palipojificha, maana nilitengenezwa mbali sana ndani ya nchi.
17Lakini kwangu ni vigumu sana kuyajua mawazo yako, Bwana, nikiyachanganya, yako na nguvu za kunishinda.Yes. 55:9.
18Yangekuwa mengi kuliko mchanga, kama ningeweza kuyahesabu. Ningaliko kwako bado ninapoamka.Sh. 40:6; 63:7.
19Nakuomba, Mungu, uwaue wasiokucha, wenye manza za damu waondoke kwangu;
20ndio wanaokutaja tu, wapate kuuficha ukorofi wao; kwa kuwa wabishi wako, hujivuna bure.
21Wachukizwao na wewe, Bwana, nisiwachukie? Nao wakuinukiao nisitapishwe nao?
22Ninawachukia kwa uchukivu usiosaza hata kidogo, ninawatazama kuwa adui zangu mimi.
23Nichunguze, Mungu, uujue moyo wangu! Nijaribu, uyajue nayo mawazo, niliyo nayo!Sh. 139:1.
24Tazama, kama nimeshika njia iendayo kwenye maumivu, unishikishe njia iendayo kwenye kuwapo kale na kale!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.