2 Wakorinto 3 - Swahili Roehl Bible 1937

Barua ya Kristo.

1Je? Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunatumia kama wengine barua za kusifiwa za kuwapelekea au za kupewa nanyi?Utukufu wa Maandiko na wa Roho.

4*Lakini Kristo ndiye aliyetupa shikizo kama hili kwake Mungu.

5Huku siko kwamba: Twafaa kuwaza neno lo lote kwa kulitoa mioyoni mwetu; kama liko, tuliwezalo, tutagawiwa na Mungu.2 Kor. 2:16.

6Naye ndiye aliyetupa kuwa watumishi wafaao wa Agano Jipya lisilo la andiko, ila la Roho. Kwani andiko huua, lakini Roho hutupatia uzima.Yer. 31:31; Yoh. 6:63; Rom. 7:6; 1 Kor. 11:25.

7Nao utumishi wa mambo yenye kuua, yaliyokuwa yameandikwa na kuchorwa maweni, ulikuwa na utukufu wake, ukawazuia wana wa Isiraeli kuutazama uso wake Mose kwa ajili ya utukufu wa uso wake uliokuwa wa kutoweka tena.2 Mose 32:15-16; 34:30.

8Je? Utumishi wa Roho hautakuwa na utukufu kuupita ule?Gal. 3:2,5.

9Kwani utumishi utupatiao hukumu ukiwa na utukufu, utumishi utupatiao wongofu utakuwa na utukufu ulio mkuu zaidi kuliko ule.*5 Mose 27:26; Rom. 1:17; 3:21.

10Kwani utukufu ule uliokuwa wa kifungufungu tu tukiufananisha na utukufu huu uzidio kabisa tutasema: Ule sio utukufu!

11Kwani chenye kutoweka kikiwa na utukufu, chenye kuwapo kitakuwa na utukufu uupitao ule.

12*Kwa kuwa wenye kingojeo kama hiki sisi hutumia mioyo isiyojua woga kamwe.

13Nasi hatufanyi kama Mose aliyeufunika uso wake kwa mharuma, wana wa Isiraeli wasipate kuutazama mwisho wa yale yaliyo yenye kutoweka.2 Mose 34:33,35.

14Lakini mawazo yao yakashupazwa. Kwani mpaka siku ya leo wakilisoma Agano la Kale, liko limefunikwa vivyo hivyo, lisiwafunukie kwamba: Limetimilia katika Kristo.Rom. 11:25.

15Ila mpaka leo mioyo yao iko imefunikwa, Mose akisomwa.

16Lakini hapo, watakapomgeukia Bwana, ndipo, kile kifuniko kitakapoondolewa.Rom. 11:23,26.

17Naye Bwana ndiye Roho; napo, Roho ya Bwana ilipo, ndipo, vyote vinapofunguliwa.

18Lakini nasi sote tunautazama utukufu wa Bwana kwa macho yasiyofunikwa, kama twauona katika kioo; ndivyo, tunavyogeuzwa, tufanane naye, tukipewa utukufu kwa utukufu, tuwe kama watu waliogeuzwa na Bwana mwenyewe aliye Roho.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help