Mashangilio 150 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumshangilia Mungu.

1Haleluya! Mshangilieni bwana hapo Patakatifu pake! Bomani mwake mwenye nguvu mshangilieni!

2Kwa ajili ya matendo yake ya nguvu mshangilieni! Kwa ajili ya ukuu wake mwingi mshangilieni!

3Kwa kuvumisha mabaragumu mshangilieni! Kwa kupiga mapango na mazeze mshangilieni!

4Kwa kupiga patu na kucheza ngoma mshangilieni! Kwa kupiga vinanda na mazomari mshangilieni

5Kwa kupiga matoazi yaliayo vizuri mshangilieni! Kwa kupiga matoazi yenye mavumo sana mshangilieni!

6Na wamshangilie Bwana wote wenye pumzi! Haleluya!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help