1Siku zilipopita nyingi, neno la Bwana likamjia Elia katika mwaka wa tatu kwamba: Nenda kumtokea Ahabu! Kwani nitanyesha mvua katika nchi.
2Ndipo, Elia alipokwenda kumtokea Ahabu, lakini njaa ilikuwa ngumu huko Samaria.
3Ahabu akamwita Obadia, mtumishi wake wa nyumbani, naye Obadia alikuwa mtu aliyemwogopa Bwana kabisa.Mvua inanyesha kwa kuomba kwake Elia.
41Elia akamwambia Ahabu: Nenda, ule, unywe! Kwani nasikia uvumi wa mvua.
42Ahabu alipokwenda zake huko juu kula na kunywa, Elia akapanda Karmeli pembeni, akainama chini na kuuweka uso magotini.Yak. 5:18.
43Akamwambia kijana, aliyekuwa naye: Panda, uchungulie upande wa baharini! Akapanda, akapachungulia, akasema: Hakuna ninachokiona, akamwambia: Rudi mara saba!
44Alipofika mara ya saba akasema: Nimeona kiwingu kidogo kama kiganja cha mtu, kinatoka baharini. Akamwambia: Nenda kumwambia Ahabu: Tandika farasi, ushuke upesi, mvua isikuzuie!
45Punde si punde, mara mbingu ikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua kubwa. Ahabu akapanda garini, akaja Izireeli.
46Lakini mkono wa Bwana ukamjia Elia, akajifunga viuno vyake, akapiga mbio kwenda mbele ya Ahabu mpaka kufika Izireeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.